Puna
JF-Expert Member
- Oct 9, 2013
- 2,551
- 4,454
Maisha ni sanaa na kuishi ni maigizo tu. Dunia hii tunapita nyie mlioko maofisini kama mnaweza saidieni watu wanaoomba Msaada kwenu.Ilikuwa hivi jamaa nilikutana nae miaka mitatu nyuma mwaka 2022, ofisini kwa DC kwa yule Dada ambaye sasa hivi ni Don kule kwenye Chama cha kijani kibichi upande wa kina Mama yaani UWT.
Mimi nilikuwa na project yangu na Yeye ya kwake, stori za hapa na pale jamaa kanigusia inshu iliyomleta na mimi yangu kumbe zinafanana Bwana, tofauti yake kuwa Yeye alikuwa anaomba kibali Cha kuingia ndani ya Wilaya mimi nilikuwa naomba sapoti yake maana alinipromise nije nimuone. Jamaa alikuwa na ufadhili wa makampuni kadhaa na baada ya kunisikiliza kumbe inshu yangu ilikuwa ya moto yaani nikiiweka mezani kwa wale jamaa zake tutakuwa tumetoboa. Tukapanga mihadi ya kukutana tena tukafanya hivyo kama mara tano kwa siku tofauti tofauti.
Inshu ikaiva jamaa akaanza kona simu hapokei kila nikimcheki anakata simu,miezi ikakata Mwisho wa siku akanitumia meseji usinisumbue akaniblock. Sasa jana mabosi wote wamesafiri ofisi nimekabidhiwa mimi, naona jamaa anakuja na mgeni anamtambulisha kuwa huyo ndie boss eleza shida yako. Nikamkakaribisha kucheki sura lo! Kama nimewahi kuiona sehemu hivi, si mwamba akajitambulisha asalale ni yule yule jamaa.
Si unajua waswahili wanamsemo wao kuwa mla ndizi mwepesi kusahau ila mtupa maganda hawezi kusahau. Roho mbaya ni malezi mimi sijalelewa kuwa na roho mbaya, sikumkubusha nikamuacha aeleze shida yake, kumbe kaleta bidhaa zake nikamkabidhi kwa jamaa akamzungusha akauza akamaliza akapewa oda zingine Leo kaja kaleta mzigo mwingine kauza kamaliza kaja kuaga nikamwambia kila la kheri ndugu.
Kasepa,nilichojifunza kuwa utakayemfanyia roho mbaya utakuja kukutana nae tu mahali huwezi kuondoka utakutana nae. Kama unaweza kumsaidia mtu Kutokana na nafasi yako hapo ofisini saidia tu.