Nyie mnatibua tu nyongo za wasionacho a.k.a walalahoi.......
Kuna mahali nimesikia (sikumbuki vizuri ni mkoa gani) kuna mahabusu wamevua nguo kupinga kusoteshwa rumande miaka kadhaa kwa kesi kama za kukutwa na bangi na mirungi.....
Huyu aliyepitisha nusu tani ya malighafi ya cocaine uwanja wa ndege anapeta uraiani na anapata air time za kubwabwaja anavyotaka....kana kwamba faini aliyolipa huko SA imehalalisha alichokifanya uwanja wa ndege wa Tanzania.
Nadhani ni bora angepiga kimya, apige tu picha za makalio yake, atuwekee mitandaoni tuburudike...