Aliyenipa mzigo wa unga alivaa kininja

Aliyenipa mzigo wa unga alivaa kininja

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
‘VIDEO queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’, amefunguka kuwa aliyempa mzigo wa unga na akakamatwa nao nchini Afrika Kusini, alikuwa amevalia kininja, hali iliyomfanya ashindwe kumtambua.

Taarifa za uhakika kutoka vyanzo vyetu makini katika kikosi kazi cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya nchini (Task Force), zinasema kuwa mwanadada huyo alipofika katika nchi hiyo, alipigiwa simu na mtu ambaye hamjui aliyemwambia kuwa atapewa mzigo, hivyo ajiandae kuupokea.

[/COLOR][/FONT][/SIZE]


MASOGANGE1.jpg

‘Video queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’.

“Alidai kuwa kuna mtu aliyevalia kininja alifika eneo alilokuwepo uwanjani pale ambaye hakumsemesha badala yake alimpatia mzigo wa unga ambao ulikuwa kilo 150 ambao hapa kwetu ni madawa ya kulevya na kuondoka kusikojulika,” kilisema chanzo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alipohojiwa na gazeti hili alithibitisha kuwa Masogange aliwaeleza polisi wa Afrika Kusini kuwa aliyempa unga ule ni mtu aliyekuwa amevalia kininja.




“Unajua watu hawa wanaojihusisha na madawa ya kulevya wana mbinu nyingi na wamekuwa wamejiandaa kwa lolote litakalotokea. Naamini alisema vile ili kukwepa kushurutishwa kumtaja aliyempa.

“Aliwaambia kuwa mtu huyo alimpa mabegi yale palepale uwanjani na hawezi kumtambua kwa sura labda kwa fulana aliyokuwa amevaa kwa sababu alikuwa amevaa kininja,” alifafanua Kamanda Nzowa.

Alisema unga huo ulifanyiwa uchunguzi kwa mkemia mkuu wa serikali wa nchi hiyo na ikagundulika kuwa si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine ambayo si unga ila ni kemikali hatari ambayo ikichanganywa na dawa nyingine hupatikana unga halisi wa madawa ya kulevya.

Aliongeza kuwa, mtu yeyote akikamatwa na malighafi kama hizo hapa nchini adhabu yake haizidi faini ya shilingi milioni 5 au kifungo cha miaka 30 ama zaidi.









[/FONT]
 

Kweli hii NCHI imeharibika... Yaani waandishi wa HABARI kweli wanakusanyika kuusikiliza UTUMBO anaousema huyu MWANADADA?

She belongs to JAIL... sio kutupigia picha za UMBO LAKE...

Hatutaweza kuendelea kama vitu kama hivi ndivyo vinavyopamba HABARI ZERU ukurusa wa MBELE...
 
Vaa yake ni uendawazimu mtupu! Na eti upewe kitu na mtu ambae humjui na wewe ukubali kubeba si ndio uendawazimu?

Waandishi wa habari andikeni mambo ya maana sio uendawazimu kama wa huyu MPUUZI.
 
Vaa yake ni uendawazimu mtupu! Na eti upewe kitu na mtu ambae humjui na wewe ukubali kubeba si ndio uendawazimu?

Waandishi wa habari andikeni mambo ya maana sio uendawazimu kama wa huyu MPUUZI.
Hakuna habari za maana za kuandika Vinginevyo Gazeti lako litakuwa na kurasa mbili tu
kwa sababu kama utaandika habari za Bunge ndio balaa kabisa utajikuta unarudia kuandika
matusi na mipasho tu ndio maana Chidi Benzi alipoulizwa kwanini unaimba matusi naye akauliza
unanishangaa mimi kuimba matusi mbona wabunge wanatukana?

 
Hebu mleteni kwangu nimhoji vizuri akiwa kavaa hivyohivyo.Nchi hii upuuzi utaendelea tu kama tutaendelea kuwa na viongozi kama hawa tulionao sasa.
 
Kwa hiyo kupewa na kukatwa na malighafi hatari itumikayo kutengeneza madawa ya kulevya si kosa kisheria?
Mbona mtu huyu yupo huru sasa?
 
Hiyo vaa yake tu inaashiria kuwa ubongo wake umejaa makamasi...
 
Eti hizi ndo habari pendwa kwenye gazeti pendwa. Upuuzi mtupu. Zimaaaaaaa
 
Simu alipigiwa na nani?

Mzigo aliambiwa aukabidhi kwa nani?

South alikwenda kwa shughuli gani?

sidanganyikii..
 
Huyu mtu wampime akili zake nadhani si sawa kabisa
 
kwanza huyu dada walisema amekamatwa na efedrine.
ni kiungo cha dawa kinachotumika kutengenezea madawa ya kulevya..alafu mbona wakati ule walisema waalikamatwa na kilo nyingi mzigo ukawa kwenye mabegi...na lazima muelewe kwa south afrika kesi hiyo ina fine...its not a big deal angekamatwa na heroin au kokain mziki angeuona
 
Yaan kajibu mashuzii hivi hao waandishii wamesoma kweliii????
 
embu aache kutudanganya hapa yeye atakubalije kubeba mzigo asioujua na hamjui aliyempa? muuza madawa tu huyo huo ndio ukweli hata kama walimtoa.
 
yaani uvae kininja kwenye uwanja wa ndege askari wanakuangalia tu wala watu hawakushangai inaingia akili hii kitu kweli
 
Thread hii inaniacha na maswali mengi bila majibu. Only simple minds will take it.
 
bora ukose mali upate akili! hizo pumba alizoongea hapo hta mtt mdogo haziwezi kumshawishi
 
Back
Top Bottom