Aliyenishauri niingie kwenye kilimo cha parachichi hapa Njombe aliniingiza chaka, nimepoteza fedha na muda

Ni kweli,madalali kwenye mazao mengi hapa Tanzania ndio wenye pesa ndefu,nakumbuka wakati ule Magufuli alivyopambana nao kwenye korosho na hatimaye akachemka...
 
Mkulima analalamika soko gumu la parachichi wakati hapa nilipo ka parachichi kadogo kanauzwa 2000 kiufupi Kuna uhaba wa parachichi sielew sijui shida Iko wapi.
Katika hiyo bei ya parachichi moja kuuzwa shilingi 2000, unajua mkulima anapata shilingi ngapi?
Kwa haraka haraka unaweza kukuta mkulima anavuna chini ya shilingi 500.
Hii inakupa picha gani?
Mkulima anatumika kuwatajirisha watu wengine (middle men) huku mteja akiendelea kufirisiwa na hao watu wengine.

Siku mkulima akiweza kukutanishwa na mteja moja kwa moja, mteja ataweza kulinunua (kwa furaha na amani) parachichi hilo hilo kwa shilingi 1000 na mkulima atafurahi mnoo kuuza kwa hiyo bei ya 1000.
 
Mkulima analalamika soko gumu la parachichi wakati hapa nilipo ka parachichi kadogo kanauzwa 2000 kiufupi Kuna uhaba wa parachichi sielew sijui shida Iko wapi.
Kujua soko na kutegemea serikali,kuna Jamaa Njombe anasifia na magari yake kaandika,Shikamoo parachchi:!
 
Kuna shida gani ukifuga hao ng'ombe chini ya kivuli cha parachichi huku ukiendelea kuvuna parachichi kwa kutumia organic manure kutoka kwa mbuzi na ng'ombe? Sijui kwanini watu wa hivyo ndio mnapewa hela 🤣🤣🫡
 
Kabisa mkuu.
 
Pole mkuu, (Kamwene) jamaa wanaacha mbao shambani hamna anayebeba Fanya tafakuri upya rutuba inatosha hapo ila sharti uelewe namna ya kulima hapo.
 
Kilimo cha maparachichi ni kama kilimo cha lubricant oil technolojia inabadilika mdau husisau ila nimecheka sana kwan nani alikushaur ?
 
Mkipata kiwanda cha kuchakata parachichi hata ambazo hazikidhi standard za kimataifa mtanufaika saaana
 
Kuna watu wengi wanajuta huko Njombe
 
Safi sana kwa kufanya maamuzi.

Watanganyika mnaendelea kuwa masikini mkitukanwa na watawala na familia zaio tokea kupata uhuru.
 

Kiongozi
Msichanganye mada
1. Mwanyaluke alilenga soko la nje akimaanisha avune hekari pengine 50 ndani ya wiki moja maisha yaendelee;
Sasa mkianza kusema aje na parachichi, Kiriku moja kila mji.....atakuwa anafanya kazi za watu wengine

2. Bidhaa za kilimo kwa wakulima wakubwa wanahitaji wauze kwa wingi wapate fedha wafanye mambo mengine na sio kuchuuza; walio soma biashara wanajua Production & Distribution Channel
Sio kawaida ulime hekari 100 halafu uanze kuchuuza....

3. Mtoa mada alitegemea kuwepo na makampuni makubwa yatakayonunua kila kinacho zalishwa na ndio sababu anasema alitapeliwa kwa ku ahidiwa soko (wanunuzi wakubwa) kaishia kukutana na madalali/Wachuuzi...
 

Hakuna sehemu nimesema auze kwa kuchuuza mkuu, ila nilionesha uhaba na bei ya kile anachosema hakimlipi katika soko la ground
 
Ukitaka kuwa maskini nchi hii kuwa mkulima.
 
Kasema shida ni tozo za serikali sasa hapo anaweza kujipanga vipi? Akamtoe mwigulu wizarani? Ushauri inabidi uwe na tija na unajibu changamoto ya muhusika na uwe feasible kbla hatujasema jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…