Aliyepigwa ngumi hana akili na mpiga ngumi ni tahira

Aliyepigwa ngumi hana akili na mpiga ngumi ni tahira

Aliyepigwa ni mpuuzi zaidi eti mtu kapigwa ngumi anasema kapigwa kofi!
 
Msongo wa mawazo,mpiga ngumi ana mawazo na mambo mengi.Mfano alikufa amebebwa na gari,yeye anakimbizana ma gari yenye maiti.Tayari ni tatizo hilo akiwa kama mwanaume shupavu.
Kwanini Wajeda hao hapo juu wameangalia tu.

Maokoto anayopata kukimbizana na gari hizo ndiyo chanzo kupiga jamaa.Umaskini ndio chanzo.

Hakuna tajiri au mwenye pesa akafanya kazi anayofanya jamaa ya kutumikia ya kukimbizana na Wakuu wa Meza.Hayupo..
 
mkuu gumi la "kanzola" ndo laaje.. halafu me najuwa kusweka ni lumande tu kumbe hata ngumi unaswekwa?
Gumi la kanzola achana nalo, ni ngumi wanaitumia sana polisi wa msumbiji.
Sifa zake;
•Ukipigwa kifuani kama ulivuta sigara ndani ya masaa 24 yaliyopita moshi lazima utoke mdomoni.
•Kama una ugonjwa wa kudumu inakusindikiza kwa mwenyezi
 
Shobo tu kwani kulikua na ulazima wa kwenda huko?
Mtu maisha magumu hata kula hujala unakimbizana kwenye mambo yasiyokuhusu.
Watanzania tupunguze shobo 😏😏
Wapigwe tu
naunga mkono hoja

jirani yake anaweza kupatwa na msiba na asijumuike ila msiba wa mwanasiasa anajitia kimbele mbele kwa sababu kuna camera

misifa mpaka msibani
 
Watu wapo kazini wanakimbia kama watumwa, halafu unajipendeza.

Lazima kikulambe.
 
Mbona kwa hayati Magu wanaliaji walikuwa wanagaragara mpk wanazuia msafara na hawakuguswa.. huyo mlinzi ni jinga kbs!
Kwa magufuli yalikuwa full maigizo. Sukuma gang walikuwa wanalazimisha kuonyesha jamaa alikuwa anapendwa
 
Kipimo cha ustaarabu katika jamii ni vile wa wanavyo heshimiana katika maisha yao ya kila siku au hata kama wana tofauti baina yao.
Hapa kwetu mitaani ni matusi, kuzomeana, kuangalia watu wanachapana mpaka wanavuana nguo na watu wamekusanyika wanashangilia.
Kuna siku nilishuhudia mama mja mzito kajikwaa kaanguka, kicheko kilichoanguka kwa watu waliokua karibu ni ajabu tu mpaka mama mwenzie akaenda kumuokota tukamkimbiza zahanati.
Safari bado ndeeefu
 
ile ilikuwa proffessional attack
nasikia jamaa katangulia
Hata mimi naweza kuamini jamaa hakunyenyuka mana inaonekana kapigwa kwenye koo likafyatuka.

Dah! Huyo mlinzi angekuwa hata na fimbo basi ya kuwachapia wanaozidi tena miguuni, na siyo kumpiga raia konde zito hivyo!
 
Ukiangalia tukio hilo ilikua haina kabisa haja ya kumpiga jamaa. Hawa walinzi wapewe mafunzo ya kazi yao kabla hawajapewa majukumu
 
Alivamiaje? embu tujuze maana mm binafsi naona kama hakua na nia mbaya hapo...
 
Kama ndo mimi ningeojiwa ningesema yule mlinzi anamkono softi sijaumia hata kidgo nilikosa balance ndo nikadondoka ningezoa umaarufu chap tu
 
Back
Top Bottom