Aliyepindua Gabon hafai, ni fisadi kama akina Bongo

Aliyepindua Gabon hafai, ni fisadi kama akina Bongo

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Mapinduzi ya Gabon yana mfanano na mapinduzi mengine yaliyofanyika nchi za Afrika Magharibi. Hata hivyo kuna vitu muhimu vinavyoyatafautisha mapinduzi hayo na wenzao.

Brice Oligui Nguema ni mjomba wa raisi aliyempindua ambaye alichaguliwa kuwa kiongozi wa kikosi cha kumlinda raisi huyo. Tofauti na wenzake wa Niger, Mali na Burkinafarso ambao wanalilia kutendewa vibaya na Ufaransa na kuwafanya wawe kama watumwa wa taifa hilo kiuchumi. Brice yeye inaonekana amekerwa zaidi na Ali Omar Bongo kuendelea kuwa raisi wakati ni mgonjwa wa kiharusi.

Mwenyewe Brice inasemekana ana majumba kadhaa nje ya nchi na amejilimbikizia fedha nyingi za kigeni kwenye mabenki ya nchi hizo. Alipoulizwa.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na taasisi ya kuchunguza ubadhirifu ya (OCCRP) kwa familia ya Bongo iligundua Brice naye alikuwa amewekeza kwenye mradi mkubwa akilipa pesa taslimu.Alikuwa amenunua mali hizo eneo la Hyattsville jimbo la Maryland mwaka 2015 na 2018 akilipia dola milioni moja.

Alipoulizwa na waandishi wa habari alijibu kwa jeuri “I think whether in France or in the United States, a private life is a private life that [should be] respected.”

1693546254181.png
 
Na huyu ataendelea kuwa kibaraka wa magharibi, lakini shida sio ukibaraka wa magharibu au russia shida kwa afrika ni kukomesha ufisadi kuwajibisha viongozi hapo ndo tutaendelea halipo taifa la nje linalokutakia mema ya kiuchumi yote yapo kimaslahi
 
Japo Tanzania kuna makandomakando ya kiutawala hapa na pale lakini kuna stability na utulivu na amani ya kiaina.

Tushukuru kwa hilo.

Uzuri wetu wengi tuna nguvu mdomoni mikwara kibao. Tukishashiba na kuvimbiwa kande, biriani na tende tunatulia na kusahau
 
Watu waahachoka,
Sahv wameamua wanataka wezi wapya
Sio kila siku wezi hao hao tu na watoto wao

Raha ya Mwizi mpya
Anaweza kuja na mbinu mpya za wizi zinazoweza kuwa na unafuu hata mtoto wa masikini akaambulia japo makombo.
 
Gaboni ni Mali ya familia ya Bongo wao ndugu ndio Huwa wanapinduana ndio nchi pekee tangu Uhuru Duniani inaongozwa na ndugu
 
Japo Tanzania kuna makandomakando ya kiutawala hapa na pale lakini kuna stability na utulivu na amani ya kiaina.

Tushukuru kwa hilo.

Uzuri wetu wengi tuna nguvu mdomoni mikwara kibao. Tukishashiba na kuvimbiwa kande, biriani na tende tunatulia na kusahau

Ndo maana mwenge unatembezwa kwa gharama kubwa sana na walamba asali,bila mwenge kitambo sana upepo ungeshabadilika.
Mwenge ni utawala wa nchi kiroho.
Ukishamilikiwa kiroho wewe si kitu kimwili ni sawa na boya tu
 
Wote wanaoingia kwa coup huwa nao hawataki kuondoka hadi nao wapinduliwe ndo ujue uongozi mtamu.
 
Gaboni ni Mali ya familia ya Bongo wao ndugu ndio Huwa wanapinduana ndio nchi pekee tangu Uhuru Duniani inaongozwa na ndugu
Kwa hivyo na huyu ni familia hiyo hiyo.Kampindua mjomba wake.Ndio maana EU wameshapinga kuingiliwa kijeshi kubadili mapinduzi kinyume na walivyohimiza kule Niger.

EU Opposes Military Intervention

 
Niliwaandikia jana kuwa hapo kuna mchezo wa kuigiza, hakuna mapinduzi.

Rais aliyepinduliwa ndiye aliyeulizwa kiongozi awe nani badala yake? Kuna mapinduzi hapo?
 
Back
Top Bottom