Aliyeshiriki kuchanganya udongo wa Tanganyika, Zanzibar afariki

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1692788713478.png

Khadija Abbas Rashid (74) miongoni mwa walioshiriki kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar amefariki dunia jana Jumanne Agosti 23, 2023 nyumbani kwake Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano ambapo wametoa taarifa hiyo katika mitandao yao mbalimbali ya kijamii.

Marehemu alihusika katika tukio hilo la mfano la kuchanganya mchanga Aprili 26, 1964.

Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Julius Nyerere na Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Abeid Karume ziliungana na kuunda Tanzania.
 
Alale salama. Ila siwaelewi kabisa hawa wazee waliokuwepo kitambo hiko. Kwanini hawaongei lolote. Kwanini wasiitishe interview watoe maoni yao. Si lazma current affairs anything sweet watupe.

Sio iwe kama ile documentary ya yule dada alikua bbc. Something clean as a story. Ona sasa anapumzika na utamu wote.

(Samahani kama nitamkwaza mtu)
 
View attachment 2726127
Khadija Abbas Rashid (74) miongoni mwa walioshiriki kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar amefariki dunia jana Jumanne Agosti 23, 2023 nyumbani kwake Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano ambapo wametoa taarifa hiyo katika mitandao yao mbalimbali ya kijamii.

Marehemu alihusika katika tukio hilo la mfano la kuchanganya mchanga Aprili 26, 1964.

Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Julius Nyerere na Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Abeid Karume ziliungana na kuunda Tanzania.
Kafara linafikia tamati
 
Hivi kumbe mwanamke ndo alikuwa Mzanzibar?
Basi Sawa.
 
Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Julius Nyerere na Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Abeid Karume ziliungana na kuunda Tanzania.
Waliua Tanganyika na watamganyika na kuiacha Zanzibar ikiendelea na jina lake na heshima ya watu wake.

Huu muungano ulikuwa na dosari nyingi sana.
 
Mwendo amemaliza japo huo Muungano mpaka kizazi hiki hakikuwahi kufaham faida zake na umuhimu wake.Hizi Media zingenufaika nazo hiyo elimu zikatufikia sisi ambao mpaka asaivi hatuelewi huu Muungano unafaida gani.
 
Hii inashiria nini kwa sisi Watanganyika?hasa katika kipindi ambacho tunadai bandari zetu zisiuzwe.
 
Apumzike Kwa Amani
Na Mwabukusi Anapata Nguvu Zaidi Ya Kuipambania Tanganyika Maana Wachanganya Udongo Ndio Wameishia Hivyo,au Kuna Waliobaki?
Tumpe Taarifa Wakili Wetu Msomi.
 
Natanguliza pole kwa wafiwa. Hawa wanahistoria wa muungano katika maadhimisho ya muungano ya mwaka 2010 waliletwa pale uwanja wa uhuru jijini dar es salaam tuwashuhudie kwa macho kuwa ndio hao walioshiriki katika zoezi la kuchanganya udongo wa tanganyika na zanzibar. Walikuwa na watu wazima tofauti na enzi hizo wakiwa vijana. Historia na siasa zitawakumbuka daima
 
Wamiliki wa muungano wanaondoka kwa nyakati tofauti.
 
Back
Top Bottom