Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Januari 3,2025 lilipokea taarifa kutoka kwa Uongozi wa Shule ya Baobaob iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani ya kutengenezwa na kusambazwa katika Mitandao ya Kijamii picha mjongeo za utupu zenye maudhui machafu kimaadili lakini pia ni kinyume na Sheria za nchi.
Picha hizo chafu na zisizo za kimaadili, waliotengeneza waliunganisha na baadhi ya Majengo ya Shule ya Baobaob ili kuaminisha umma kuwa vitendo hivyo vinafanyika shuleni hapo.Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya uchunguzi na limefanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye uchunguzi wa kitaalam ulisaidia kumfikia na kumkuta na picha hizo na kifaa cha kielekroniki ambacho alikuwa akitumia kusambaza picha hizo chafu.
WITO
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa onyo kwa watu wenye tabia kama hizo za kutengeneza na kusambaza picha kama hizo kwa malengo ya kuchafua wengine au taasisi kwani mkono wa sheria lazima utawafikia na hata kama hautawafikia mapema wataendelea kupata shida ya kujificha na kuacha kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo.