Aliyesoma Elimu ya Masafa(ya Mtandao) kama Open University akikutana na waliosoma UDSM, SAUT na Mzumbe anatakiwa Kuchangia lolote?

Aliyesoma Elimu ya Masafa(ya Mtandao) kama Open University akikutana na waliosoma UDSM, SAUT na Mzumbe anatakiwa Kuchangia lolote?

Inawezekana vipi 'Wanamume' wameumia Darasani huko UDSM, SAUT na Mzumbe halafu Wewe uliyesoma OUT ( hapo Biafra ) na Kupata Degree ( Shahada ) yako tukikutana Vijiweni uwe na la Kuchangia?

Elimu ya Masafa 'inamheshimisha' Mtu kweli au ndiyo labda 'inamdharaulisha' mbele ya wale Waliohudhuria 'Lecture Sessions' zote kwa miaka Mitatu au Minne na Kupata Bachelors zao walizozihangaikia Darasani huku 'sometimes' wakipata 'Sapu' za Kutosha tu.
Walichosomea ni hicho hicho, haijalishi mazingira.
 
Mtoto wa geti na mtoto wa uswazi nani mjanja zaidi anajua mengi zaidi.
OUT still wapo vizuri sana kwenye reasoning maana Ili ufaulu ni lazima ujipinde kweli.
Miaka ya nyuma nikisoma A level mwezi mzima Hakuna Mwalimu darasani tulikuwa tukisema tupo likizo tulikuwa tukijisomea wenyewe kwa kudiscuss, ikifika likizo ndo tunasema tunakwenda shule likizo KILA mmoja alipambana kutafuta tuition tukirudi shule ndo likizo yetu tunapiga msuli hatari pekee yetu KILA mmoja na aliposomea tuition mikoa tofauti tofauti robo tatu ya darasa wote walienda vyuo vikuu.
 
Nimempiga brashi jamaa yangu alikuwa anachukua Masters hapo OUT aisee kile chuo kipo vyema madesa ni ya uhakika yani! Uzuri unajisomea mwenyewe personal pale hamna kutegea yani😅
Ngoja nikapige pale huku nikisaka hela mambo ya fingerprint kama Mzumbe nani anataka yaani unanitaka nikae darasani wakati na akili Acha maisha yaendelee tukutane kwenye pepa na ada,mambo ya kuchungana ya nini,Mimi nataka cheti tu niongeze CV wakati wa mazishi.
 
sasa hizi fani kama sheria, ualimu, public administration, political science nk unakaa darasani ili iweje.....unapiga tu mishemishe zako usiku ukirudi home unawasha computer unasoma....hakuna tofauti..

labda kidogo wanaosoma engineering wanaweza kusema kitu....ila wengine haijalishi umesoma online au live mko sawa tu...
 
tunakoendea hizi fani zenu za siasa siasa zote zitakuwa online labda mitihani ndio mtaambiwa muende huko vyuoni....

Engineering na ukomandoo pekee ndio vitabaki kuwa live darasani na wakufunzi..
 
Anaongea vizuri sana, tena anawatoa njeee!! Ukitaka kujua ubora wa elimu ya masafa ya OUT
1. Mitaala ya OUT inasimamiwa na TCU, kuhakikisha ubora unadhingatiwa! Mbona hakifutwi kama ni dhaifu?

2. Wakigraduate mfano LLB wanakwenda Law school na kukimbizana ipasavyo na hao wa conventional!

3. Wahasibu wanaomaliza mafunzo OUT wanapita bodi za uhasibu na kupata CPA na taaluma zinginezo.

4. Interview za serikali au binafsi mnachanganywa wote humo!! Mara nyingi walomaliza OUT hupata kushinda!! Hapo vipi??

5. Unajua kuna wanataaluma nguli wa hivyo vyuo ulivyotaja ambao ni zao la OUT?? Tena wanawafundisha nyie. Au niwataje??

6. OUT ni chuo bora kabisa kwa sasa ni namba moja barani Africa kwa vyuo vinavyotoa elimu masafa miongo mwa mlolongo wa vyuo kutoka mataifa bora kabisa kielimu. Hadi UNISA walikwenda OUT kujifunza??

7. OUT ndiyo taasisi namba moja kwa mwaka 2021 Tanzania kwa matumizi bora ya TEHAMA inayotolewa na tume ya TEHAMA nchini. Hapo UD tupa kule, SUA kanyaga, Mzumbe sogeza vile, tuzo alitoa Mh. Majaliwa huko Arusha.

8. Imepata Recognition certificate kutoka ATU, unawajua hao?? 🤣🤣🤣

Kwa vigezo hivyo, nakuhakikishia kabisa kuwa wanaume wanaomaliza OUT wanapaswa kuheshimiwa. Akisimama mnapaswa mkae chini kwa heshima!! Wenzenu wanapiga nondo kwa malengo na si michezo yenu ya kufuata wanafunzi wakike vyumbani mwao muwakulena kuwapa alama (refer mhadhiri wa UDOM).
Kwenye university ranking, OUT ni ya ngapi?
 
SAUT-Saint Augustine University of Tanzania na OUT-Open University of Tanzania
 
Inawezekana vipi 'Wanamume' wameumia Darasani huko UDSM, SAUT na Mzumbe halafu Wewe uliyesoma OUT ( hapo Biafra ) na Kupata Degree ( Shahada ) yako tukikutana Vijiweni uwe na la Kuchangia?

Elimu ya Masafa 'inamheshimisha' Mtu kweli au ndiyo labda 'inamdharaulisha' mbele ya wale Waliohudhuria 'Lecture Sessions' zote kwa miaka Mitatu au Minne na Kupata Bachelors zao walizozihangaikia Darasani huku 'sometimes' wakipata 'Sapu' za Kutosha tu.
GENTAMYCINE nimekuja kwa kuchelewa. Maishani kuna kujifunza na kufundishwa. Tunapofundishwa tunapata maarifa kidogo sana ukilinganisha na tunavyojifuna.
Tunapojifunza mazingira, asili yetu na utu wetu unakusanyika pamoja kutafuta maarifa.

Tunapofundishwa tunalishwa werevu na ukengeufu wa mwalimu.

Daima nasema unyago na elimu ya ujando na ya jadi vidumishwe. Hii elimu ndio ilileta wakulima hodari, wafugaji mahiri, wawindaji madhubuti nk.

Nakaribisha mawazo na maoni yako. Vijana wa leo hawakujui wanadhani wewe ni mjivuni, mtukanaji ec. Lakini wewe ni bonge la muungwana
 
Mtoa post uelewa wako na wa kondoo ni sawa kabisa. Wengi wanaosoma out wana uelewa kuliko wanaosoma fresh sababu wengi unakuta wanachosoma wana kipractice kila diku. Mm nimesoma darasani udsm na ninasoma out kwa sasa hivyo nina ulewa mzuri kuliko wewe
 
Afu walimu wa out ni very humble na wana customer care ya kimataifa tofauti na wakiwa na undergraduate wa incampus huwa hawajali sana ila out mwalimu ukimwambia sijaelewa sehem unamwona kabisa inamnyima raha na anakuhudumia frendly
 
Mtoa post uelewa wako na wa kondoo ni sawa kabisa. Wengi wanaosoma out wana uelewa kuliko wanaosoma fresh sababu wengi unakuta wanachosoma wana kipractice kila diku. Mm nimesoma darasani udsm na ninasoma out kwa sasa hivyo nina ulewa mzuri kuliko wewe
The same.. Bachelor Udsm.. now Masters OUT aisee usidanganyike eti OUT hakuna quality.. Naona wapo vizur tu..

Halafu ubora wa mtu ndo una matter
 
Aisee mpo dunia ya karne ya tatu. Sasa hivi hadi vyuo top class wanasoma kwa mtandao! Dunia imebadilika ndugu, kuna certification zipo online kuzipata unatoa jasho kweli na zinakupa elimu ambayo huwezi kuipata kwenye vyuo vyetu hivi. Mfano leo ukitaka kubobea kwenye Financial Modelling huwezi kupata kwenye vyuo vyetu hivi na huko online certification zake si mchezo na very expensive.
 
Mimi nna swali; mtu akipiga degree online chuo cha mambele let's say Liverpool university...Na mwingine akakomaa UDSM.
Yupi ana advantage kwenye Soko la ajira?

Na cheti cha online course huwa kinaainisha huyu mtu alisoma online au darasani?
 
Inawezekana vipi 'Wanamume' wameumia Darasani huko UDSM, SAUT na Mzumbe halafu Wewe uliyesoma OUT ( hapo Biafra ) na Kupata Degree ( Shahada ) yako tukikutana Vijiweni uwe na la Kuchangia?

Elimu ya Masafa 'inamheshimisha' Mtu kweli au ndiyo labda 'inamdharaulisha' mbele ya wale Waliohudhuria 'Lecture Sessions' zote kwa miaka Mitatu au Minne na Kupata Bachelors zao walizozihangaikia Darasani huku 'sometimes' wakipata 'Sapu' za Kutosha tu.
Kama mawazo haya yanatoka ndani ya kichwa chako na umesoma hivyo vyuo unavyovidhania kuwa ndio imara academically kuliko OUT basi kuna haja kubwa sana ya kuangalia upya elimu inayotolewa na hivyo vyuo vyenu....
 
Tupo katika mazoea ya kishamba sana, ukweli ni kwamba the age if information imerahisisha kila kitu.
Ukiwa Nyumbani unawasha computer yako unahudhuria lecture ya Yale university unasikiliza kwa makini vile profesa anamwaga madini yake kuliko profesa wangu wa UDSM SUA,SAUT ,MUM nk.
Nilipokuwa chuo nuli enjoy sana lecture za profesa lewis wa MIT, that guy is the GURU of teaching physics wf!
Yani mtu wa OUT akizama akasikiliza lecture za Yale,MIT, Birmingham, Oxford ku@@ma&&maae!! wewe ulieshinda vingweta vya chuo humkuti kabisa.
Nakumbuka niliweza kumaster quantum physics( particle in a box) kwa kufuatlia kwa adabu lecture moja ya Mjapani/mmarekani acha kabisa, darasani nilikuwa naona kama napoteza muda(levture alitushsuri tukariri baadhi ya vipengere, ujinga kabisa).
Kati ya kitu ambacho wanafunzi wa kisasa wana enjoy ni internet kuna kila lecture kila mada huna haja ya kukomaa na darasani tu.
Nakumbuka nimewaahi otea notes na maswali mtandaoni kumbe lecture kakopi na kupest 100% mtandaoni.
Nakwambia muandika mada, ma lecture wa kibongo wana copy paste kila kitu mtandaoni.
Nimefanya utafiti na ukibisha ntakutajua code za kozi za vyuo vyetu na wapi wamekopi note.
Muandika mada inawezejana umesoma chuo miaka ya 2000 kurudi nyuma internet haijawa na nguvu hivyo unamawazo ya kizamani.
 
tunakoendea hizi fani zenu za siasa siasa zote zitakuwa online labda mitihani ndio mtaambiwa muende huko vyuoni....

Engineering na ukomandoo pekee ndio vitabaki kuwa live darasani na wakufunzi..
Sio engineering zote lazima ukae darasani. Software engineers wengi wamesoma kwa njia ya masafa.
 
Back
Top Bottom