Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema amemuengua Bonaventura Peter Ndekenja wa chama cha NRA aliyemtumia baruapepe akieleza nia yake ya kutaka kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu yeye si mbunge.
“Yeye si mbunge hivyo chama chake kilipaswa kuwasilisha jina lake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuthibitisha kama anakidhi vigezo vya kuwa mbunge. Kwa kutofanya hivyo, ndugu Ndegenja amekosa sifa,” amesema Kagaigai.
Sababu nyingine iliyomwondoa mtiania huyo aliyeamua kujaribu bahati yake, Kagaigai amesema baruapepe yake ilimfikia saa 12 jioni badala ya saa 10 jioni, muda wa mwisho kuwasilisha maombi ya kuwania uspika.
Alipopewa muda wa kujieleza mbele ya wapiga kura wake, Ndugai anayewakilisha Jimbo la Kongwa amesema atatenda haki kwa kila mbunge katika uongozi wake.
Jumla ya wabunge 263 wamepewa karatasi za kupiga kura ama kumchagua au kumkataa Ndugai kuwa mkuu wa mhimili huo wa dola.
Ndugai anapigiwa kura kuwania muhula wa pili wa kuliongoza Bunge hilo huku akiwa na uzoefu wa kuwa Naibu Spika kwa muhula mmoja pia.