Aliyetoa Tsh. Milioni 30 na Ng'ombe 30 kama mahari hana tofauti na wewe uliyetoa mahari ya Tsh. Milioni 1. Wote akili zenu zinafanana

Aliyetoa Tsh. Milioni 30 na Ng'ombe 30 kama mahari hana tofauti na wewe uliyetoa mahari ya Tsh. Milioni 1. Wote akili zenu zinafanana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Hamjambo wote!

Kuna watu wanafurahisha Sana.
Ati wanamshangaa na kumsimanga Azizi Ki kwa kutoa Mahari 30m na Ng'ombe 30 na kumshutumu na kumkejeli kwamba ni mshamba sijui kanunua gazeti la Juzi, sijui ganda la Muwa la Jana, oooh! Jamaa kaoa single mother kwa gharama kubwa. Yaani blah blah!

Sisi Watibeli hatuoni tofauti yoyote ya Mtu aliyetoa Mahari Milioni 30 au Milioni 100 na Yule ambaye ametoa Mahari ya Laki Nane. Wote ninyi mpo kundi Moja.

Wakati Mnamshangaa mwenzenu kwa kutoa Milioni 30 Sisi Watibeli ndio tunashangaa zaidi kwa nini mnatoa hizo Mahari. Kwa kweli ni Moja ya mambo ambayo yanawafanya wanadamu wawe viumbe wenye Vioja.

Mwanamke yeyote aliyetolewa Mahari bila kujali nafasi yake. Ni binadamu aliyethaminishwa kama bidhaa Fulani.

Mtu hatolewi MAHARI
Mtu hajawahi kutolewa MAHARI
Na ndio maana wanaume wengi hawatolewi MAHARI kwa Sababu wao ni WATU.

Mahari ni biashara ya kumnunua binadamu mwingine ili aje awe chini ya Miliki yako.

Wenyewe watoa Mahari ukiwaambia kuwa wanafanya biashara ya kuuza na kununua binadamu wakike. Wanakukatalia. Sio biashara

Alafu Muda huohuo ukienda kutoa Mahari(kununua mwanamke) utasikia wakijadili thamani ya huyo Mwanamke.
Ooh! Binti yetu ni mweupe! Mzuri na tumemlea vizuri.
Tumemsomesha hivyo utatoa Milioni tano.
Alafu vile vianamke visivyo na mvuto wowote vitauzwa hata kwa Laki Tatu au Milioni Moja. Kwamba vina thamani ndogo ukilinganisha na wale mabinti warembo wenye rangi yenye kuvutia machoni au Waliosoma na kuwa na elimu Kubwa.

Ukiwauliza wanaokataa Hamisa Mobeto kwa nini asitolewe hiyo Milioni 30 na Ng'ombe 30 Sababu wanazotoa utagundua ni Kwa nini Watibeli hatutoi Mahari na Wala Binti zetu hawatolewi MAHARI(hawauzwi)

Sio HAKI kuuza binadamu Wala sio HAKI kununua binadamu lakini sio HAKI ikiwa binadamu hao wanautu ndani Yao.

Haya ngoja tuendelee kushangaana
 
Mahari ni ujinga,yaan watu umewasaidia kuwaondolea mzigo nyumbani afu tena uwalipe,huo ujinga nilishaukataa
Yale si malipo mkuu. Ni kama ishara ya uhalali unaopewa na ndugu/wazazi kwa binti yao kukuhudumia mahitaji yako ya kimwili, kiuzazi na kuendeleza ukoo wako.

Ni kautaratibu tu ka kuheshimiana baina ya koo na koo. Ni vile tu tumepuuza mila na desturi zetu na kugeukia umagharibi otherwise ulikuwa utaratibu mzuri mno.
 
Kulipia mahari ni uhuni.
Naunga mkono hoja...😊

😃😃

Unaenda. Unaambiwa;.

Wakwe: Binti yetu ili umuoe itakupasa ulipe Milioni Mbili.
Wewe: mmmh! Mbona nilisikia Dadaake hakununuliwa kwa pesa yoyote.
Wakwe: unatukosea adabu Kijana.
Wewe: samahanini wazee; Mimi Nina Laki Tisa
Wakwe: Laki Tisa? Umeshuka Sana. Laki Tisa hainunui hata pikipiki.
Wewe: Kwani Milioni Mbili inanunua nini Mpaka mkanitajia?
Wakwe: naona huyu amekuja kutodhihaki. Mtoeni hapa.

Wewe: Binti yenu hata bikra Hana, natoaje Milioni Mbili.
Wakwe: Wewe Mamaako aliolewa Akiwa na Bikra?
Wewe: Mngemuuliza yeye sio Mimi.
Wakwe: embu tutolee Nuksi zako hapa
 
Fuatilia vzr tangu zama za zamani kama Watibeli walikuwa hawana utaratibu wa kupeana vitu vitu/zawadi as a sign of goodwill kabla ya ndoa

Watibeli tunatoa zawadi na sio MAHARI

Mahari sio zawadi ni gharama au bei iliyothaminishwa na wazazi wanaotaka kumuuza Binti Yao.

Zawadi unatoa wewe mwenyewe pasipo kutajiwa ulete zawadi gani. Ni Jambo la hiyari ya mtu kutoa kitu kulingana na mahusiano na mtu husika
 
Back
Top Bottom