Aliyetoa Tsh. Milioni 30 na Ng'ombe 30 kama mahari hana tofauti na wewe uliyetoa mahari ya Tsh. Milioni 1. Wote akili zenu zinafanana

Kwa Watumwa Mahari ni lazima.
Ila kwa Watu hakuna msamiati unaoitwa Mahari.
Tubaki unavyoamini nibaki na ninavyoamini ila
Kama wewe huwa unasoma Biblia
Nenda kasome Laban alichomfanyia Jacob Kwa Rachel 😀😄😃.
 
Watibeli tunatoa zawadi na sio MAHARI

Mahari sio zawadi ni gharama au bei iliyothaminishwa na wazazi wanaotaka kumuuza Binti Yao.

Zawadi unatoa wewe mwenyewe pasipo kutajiwa ulete zawadi gani. Ni Jambo la hiyari ya mtu kutoa kitu kulingana na mahusiano na mtu husika
Ni lugha tu mkuu. Kama zilivyokuwa vzr dini zetu za kiasili za Kiafrika kabla ya kuingiliwa na dini za kigeni,huo nao ni utaratibu mzuri pia. Ni tukio lililokuwa linafanyika kwa upendo,mshikamano,amani na furaha. Ndio msingi wa mama zetu unaowaona as real wife materials. Ndio msingi wa ndoa zilizokuwa imara.
 
Kumuuza mtu huwezi kuita ni tukio la Upendo.

Ingekuwa zawadi hapo Sawa.
Mahari sio zawadi kwenye tamaduni nyingi hasa tamaduni za kishenzi
 
Tubaki unavyoamini nibaki na ninavyoamini ila
Kama wewe huwa unasoma Biblia
Nenda kasome Laban alichomfanyia Jacob Kwa Rachel 😀😄😃.

Laban alikuwa Mpagani na mwenye Mila za kishenzi.

Rachel mwenyewe anasema Baba Yao aliwauza. Kasome vizuri Biblia utamsikia Recho akisema Jambo hilo. Au nikusaidie Aya
 
Yale si malipo mkuu. Ni kama ishara ya uhalali unaopewa na ndugu/wazazi kwa binti yao kukuhudumia mahitaji yako ya kimwili, kiuzazi na kuendeleza ukoo wako.

Ni kautaratibu tu ka kuheshimiana baina ya koo na koo. Ni vile tu tumepuuza mila na desturi zetu na kugeukia umagharibi otherwise ulikuwa utaratibu mzuri mno.
kama sio malipo kwanini kuna kubargain?
 
Mahali sio utumwa Wala sio biashara .

Uislamu unasisistiza mahali kiwango Cha chini ndio maana hata ndizi Moja yafaa kuwa mahali ikiwa Mwanamke ataridhia.
 
Fuatilia vzr tangu zama za zamani kama Watibeli walikuwa hawana utaratibu wa kupeana vitu vitu/zawadi as a sign of goodwill kabla ya ndoa
Basi hizo goodwill/zawadi zilipaswa kutolewa kwa pande zote maana wote ni wanadamu walio na thamani waliopata malezi ya thamani.
 
kama sio malipo kwanini kuna kubargain?
Nachomaanisha ni kuwa si malipo yanayowakilisha thamani ya mwanamke, ni kitu kinachotolewa kama ishara ya heshima kwa upande wa pili kwa kukuza binti atakaye endeleza ukoo wako. Ndo maana haikupi uhalali wa umiliki wa binadamu kama bidhaa. Na ukiwa na mshenga mtu mzima mwenye busara anaweza toa ushawishi bila fedha, akaenda hata na fimbo ya mzee wa boma kulingana na tamaduni.
 
Yale si malipo mkuu. Ni kama ishara ya uhalali unaopewa na ndugu/wazazi kwa binti yao kukuhudumia mahitaji yako ya kimwili, kiuzazi na kuendeleza ukoo wako.

Ni kautaratibu tu ka kuheshimiana baina ya koo na koo. Ni vile tu tumepuuza mila na desturi zetu na kugeukia umagharibi otherwise ulikuwa utaratibu mzuri mno.
Na huyo binti kumbuka pia anahudumiwa mahitaji yake ya kimwili na huyo mume anayetozwa ada pamoja na kuyarutubisha mayai yake huyo binti (kumzalisha) na kuendeleza ukoo wa wakwe(yaani wazazi wake binti wanapokea zawadi ya wajukuu pia),tusipangiane aisee,hizi desturi ni upumbavu wa wanaume,wizi na utapeli.
 
Huku Kenya bunge letu lilipitisha mswada wa kutokuhalalisha hiki kitendo cha mahari, wakaongezea kuwa si shuruti kutoa mahari bali kila mtu akatoe kwa hiyari yake ila ukija ukatokwa na mke au kutapeliwa husije kuisumbua serikali ukidai mahari uliyotoa.
 
Na huyo binti kumbuka pia anahudumiwa mahitaji yake ya kimwili na huyo mume anayetozwa ada pamoja na kuyarutubisha mayai yake huyo binti (kumzalisha) na kuendeleza ukoo wa wakwe(yaani wazazi wake binti wanapokea zawadi ya wajukuu pia),tusipangiane aisee,hizi desturi ni upumbavu wa wanaume,wizi na utapeli.
Mkuu, Watoto Jina wanabeba la nani? Na mke ruksa kubadili jina. Ni desturi nzuri tu ambazo tumekua nazo, sasa hivi ndo ujuaji mwingi na mambo ya haki sawa na ufala mwingine wa kutosha
 
Wala wanawake wengi hawabadili majina yao tena kama ilivyokua hapo awali.Je wajua kua kabila la wakikuyu hapa Kenya watoto hupewa majina ya wakwe?,kwa mfano mtoto mwanamme hupewa jina la mamake mke,tafakari hayo.
 
Utasemaje kwenye jamii kama za wahindi kule ambapo mahari utolea mume na familia yake lakini siyo mke?
 
Back
Top Bottom