Inawezekana kwa 2001 kule visiwani hili wazo lilifanya kazi kwa sababu mbalimbali na sababu kuu ni kutokuwa na maendeleo makubwa ya teknolojia kwa wakati huo. Inasemwa kwamba visiwani kulikuwa na mauaji ya kutisha na kikatili mno. Wasimuliaji wanadai hata waliokuwa wakikimbilia nchi jirani wengi boti zao zilizamishwa na kupoteza maisha. Ulikuwa ni ukatili usioelezeka. Imagine mko katikati ya bahari kwenye boti mnakimbia mara ghafla helikopta inasimama juu na kuanza kuwamiminia risasi..!!!!.. Hayati Ben na Mr Zero hawapaswi kusamehewa.
Miaka 24 baadae kukiwa na maendeleo makubwa ya teknolojia anajitokeza mtu na kuamua kufanya kama 2001 ili kunyamazisha watu inashangaza sana. Mwaka 2001 camera man alikuwa mtu wa kuheshimika mji mzima ila leo hii kila mtu mwenye smartphone ni "camera man". Hata utunge sheria kali kiasi gani lazima habari na picha zivuje. Kujificha haiwezekani.
Haya mauaji yameuchafua mno utawala wa awamu ya 6. Ni doa baya ambalo ni ngumu kufutika. Tofauti na mauaji mengine kabla ya tarehe 29 ni kuwa haya ni mauaji ya halaiki yasiyoangalia chama, dhehebu, rangi wala kabila. WanaCCM, Wapinzani, wakristo, waislamu hadi wapagani ni kilio. Hakuna aliyepona safari hii. Hata hao wauaji huenda wamepoteza ndugu zao pia. Yaani kwa sasa ndani na nje ya CCM watu wana machungu yasiyoelezeka.
Mheshimiwa Rais katamka mambo mbalimbali na kuahidi kufanya uchunguzi ila ninamsihi ahakikishe waliohusika wanapelekwa mahakamani. Kwa uzoefu wangu ni kuwa wauaji nao wako kwenye hatari ya kupotezwa kama walivyowafanyia raia wengine ili kupoteza ushahidi. Wakipelekwa mahakamani uozo mwingi sana utafichuka.