Aliyetufikisha Uchumi wa Kati ni Kikwete na siyo Magufuli, acheni kudanganya!

Aliyetufikisha Uchumi wa Kati ni Kikwete na siyo Magufuli, acheni kudanganya!

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Unajua hawa watu wanatufanya mazezeta aisee ukweli ni kwamba kikwete ndo alifanya Tanzania kuingia uchumi wa kati kwa hoja zifuatazo:

Kwanza kabisa kigezo cha kua uchumi wa kati mdogo unapaswa uwe na Per capita income ambayo ni dola za kimarekani $1036 hadi $4045.

Kwa uchumi wa kati mkubwa unapaswa kuwa na per capita income ambaye ni dola za kimarekani $4046 hadi $12535

Sasa wakati wa kikwete alipambana sana hadi tukakaribia point zote kuwa uchumi wa kati kabisa

Mfano mdogo tu mwaka 2014 per capita income ilikua dola za kimarekani $1030 ambapo ukitazama hapo ilibakia point 6 tu ili kufikia dola $1036 ambazo zinahitajika kuwa uchumi wa kati sasa hapo kwa lugha rahisi ni kikwete ndo alitufikisha uchumi wa kati

Jpm miaka yote mitano hakuweza zaidi ya kuongeza hizo point 6 tu nawaambia mfano jk angekua madarakani hadi 2020 Tanzania ingekua kwenye per capita income ya $2000 hadi $5000 au zaidi ya hapo maana jk alikua anaenda kiutekelezaji wa dira hii ya 2025 ambayo muasisi ni mzee mkapa ambapo alitaka ikifika 2025 Tanzania iwe tumefika $3000 na kuendelea

Pia msisahau vipaumbele vya jk 2010-2015 vilikua ni kuibua fursa za maendeleo tz ambapo pia.

2015-2020 vipaumbele vingekua ni tz ya viwanda ambavyo jpm alituaminisha ni yeye lakini hii ilikua kwenye priority ya Jk na hii sera jpm amefeli vibaya sana.

Pia 2020- 2025 vipaumbele ni kuimarisha tz katika ushindani na katika masoko ambapo ndo tunamuona mama Samia akipambana na atafanikiwa.

Pia tusisahau awamu ya nne na tatu uchumi ulikua hadi 7% lakini toka jpm kaingia uchumi ulidumaa hadi asilimia 4 kwa sababu ya sera zake mbovu.

Anayestahili kupewa sifa ni Jk kwa kutupeleka uchumi wa kati na sio Jpm maana hakuna alichofanya.

Rejea hotuba ya Jk msiba wa Rais Mkapa video[emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313]kuanzia dk ya 9 hadi mwisho kaeleza[emoji1313][emoji1313]



My take

Mnaoteseka na hizi hoja huu ndo ukweli, na ukweli utabaki kuwa ukweli na lazima usemwe,zama za kupika data, na kudanganya zimepitwa na wakati, mnaopinga leteni ukweli wenu mnaodai sasa.

Leteni hoja zenu zinazothibitisha kwamba jpm ndo alitufikisha uchumi wa kati ukweli ndo huo hakuna kitu kama hicho ashukuriwe Jk na mkapa!
 
Katiba yetu ingekuwa Kama ya Russia ingekuwa poa Sana.....
 
Uchumi wa kati ni nini? Kwamba sasa wanafunzi wanakalia viti vya plastiki? Yaani bado tunamwamini mkoloni atuwazie? Kwa nini tusifikiri wenyewe? Sisi bado tupo kwenye ujima yaani miaka 6o hatujui kesho yetu ,Madini yote tunayo,mbuga zote tunazo, uchumi wa kati unafananaje na Huo wa mwanzo ulikuwaje
 
Hahaha...mnapandia kwa migongo ya wenginee..chuma kitabaki kuwa chumaa tuu...jembee limelala..viushuzii vya mizogaa vinahangaikaa huku..hilo neno la uchumi wa kati halikuwah kutajwaa leo jembee chumaa kimelala..kimetifikisha uchumi wa kati..waswahili wanaanzaa kujamba jambaaa..mfyuuu..pelekaaa upuuzi wenu hukoo.
 
Historia ya Magufuli haitawezwa kufutwa KAMWE. Nyie wazembe , mafisadi, wala rushwa,majizi, watumbuliwaji mtaendelea kupiga kelele dhidi ya ukweli lakini hamwezi na hamtaweza kuufuta.

Magufuli atasomwa kwa mazuri mashuleni na watoto wenu na Africa nzima. Najua unachuki na sababu inajulikana kati ya hizo juu. Ila Magufuli alikuwa jembe, chuma.

Ukitaka kuamini wananchi walimwelewa angalia umati uliojitokeza kumuaga na kumzika...usijiangalie ww na wenzako mnaobwabwaja kwenye mitandao. Wenye akili zao wanajua Magu alikuwa chuma na ndiye aliyetupeleka uchumi wa kati.
 
Mwisho wa siku mtasema JPM Haujawahi kua Rais wa TZ.

Mbona mmahangaika hvyo wajukuu wa Msoga?
Nyinyi ni miongoni mwa awamu zilizokua za hovyo kuwahi tokea,hata mfagiaji wa ofisi tu aliiba na mafisadi na matapeli kama pappas MSOFE walijaa mtaani
Shetani anahangaika sana kubadilisha ukweli na ndiyo kazi yake.
 
Acheni uzuzu,uchumi upi huo wa kati, mbona watz tunakuwa wajinga hivi? Juzi nilipita vijiji vya kilolo iringa na baadhi ya maeneo ya Morogoro Ulanga, daah, kusema kuna uchumi wa kati ni wizi tu.

Maana kule kuna ufukara uliopitiliza, tembeeni muone acheni kupiga kelele za wanasiasa mitandaoni. MAISHA ni MAGUMU sana vijijini tuache utani aisee.
 
Historia ya Magufuli haitawezwa kufutwa KAMWE. Nyie wazembe , mafisadi, wala rushwa,majizi, watumbuliwaji mtaendelea kupiga kelele dhidi ya ukweli lakini hamwezi na hamtaweza kuufuta...
Unateseka sana ukweli ndo huo leteni ukweli wenu
 
Back
Top Bottom