ALIYEUNGWA NA KAHABA AMEKUWA MWILI MMOJA NAYE:

ALIYEUNGWA NA KAHABA AMEKUWA MWILI MMOJA NAYE:

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
MAKALA HII imeandaliwa na
CREEZLE FAREY
WhatsApp ME +255789407381

KAHABA : Kahaba ni neno linalotumika kumaanisha mtu anayejiuza kwa ajili ya ngono. Katika muktadha wa jamii, kahaba mara nyingi anachukuliwa kama mtu anayefanya kazi hii kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na umaskini, mazingira magumu, au uchaguzi binafsi.

Katika tamaduni nyingi, kahaba anaweza kuwa na taswira tofauti; wakati mwingine anaweza kuonekana kwa dhana hasi, lakini pia kuna maoni yanayoweza kumtazama kama mtu aliye katika hali ngumu ya maisha. Katika baadhi ya maandiko ya kitamaduni na kifilosofia, kahaba pia anaweza kuwakilisha makosa au maovu.

KUUNGWA Ama UNGANISHWA: Neno "kuungwa" ama "kuunganishwa" lina maana ya kuleta vitu viwili au zaidi pamoja ili kufanya kitu kimoja. Katika muktadha wa lugha, inaweza kumaanisha kuunganishwa kwa maneno au sentensi ili kuunda mawasiliano ya maana. 😎mpaka tuko pamoja?

SASA kwakua tumeshajua maana halisi ya kuungwa na maana kamili ya kahaba,
Basi tufunue yaliyojificha nyuma ya mchezo huu

KAHABA anajiunganisha na watu wa aina mbali mbali na wenye tabia,
Mbali mbali....
Anapokea kwanza vitu vya aina mbili

>>>PESA kwanini nasema pesa, ilipo hazina ya mtu ndipo moyo wake ulipo namaanisha hivi,moyo wa mtu umebeba matatizo mengi Sana,ikiwemo vilio vya kifamilia,unyanyasaji wa hisia aliotendewa
Pengine mkewe huwa anamnyanyapaa kumpatia unyumba,
Masononeko,huzuni,vilio vya matendo ya watoto wake,
Vilio ni vingi Sana nafsini....
Hivyo pesa huambatana navyo vyote,kwakua ndio hazina yenyewe..
Ogopa sana mtu anapokupatia pesa akiwa anakunung'unikia
Mimi Creezle Farey nimeyaona haya yote,nakuyshuhudia.
Ni
Kama HADITHI ya Askari wa jeshi aliyemwendea ELISHA aponywe ugonjwa wake,Lakini akaambiwa kuoga mtoni...
Bado alitoa pesa na vito vya thamani,vikakataliwa na ELISHA kwakuwa awali hakusadiki...
Yale maradhi yalikuwa yamejificha ndani ya ile pesa na vito vya thamani...
Hivyo mfanyakazi wa Elisha alipoamua kuiba ama kuipokea ile pesa na vito,,,yale matatizo yaliyoambatana na moyo wa yule mkuu wa majeshi,yakamrudia mjakazi.😎
√ TUHAME huko.
Kahaba anapokea matatizo mengi rohoni,kweli anashika fedha Ila ndani ya fedha hio kuna vilio vingi😎
Ni kweli anatatua mengi mwilini lakini rohoni inampeleka DIMENSION nyingi na za mbali katika UUNGU.

>>>> Anajiunga na wa watu wengi anabeba tabia nyingi tofauti,ambazo hata yeye hataelewa zinatokea wapi na kwanini amekuwa hivyo....

NDIYO maana mkeo
Akishatoka nje ya nyumba yaani familia tu ile maramoja ni KOSA kubwa Sana,maana linaenda kufungua mnyororo mrefu Sana kiasi kwamba kuukata na kuufunga mlango ni gharama ambayo hata inaweza kuzaa mauti...
Mfano: amelala na mwanaume ambaye tayari,yuko kwenye mnyororo wa malaya,hio tabia nawewe mwanaume lazima ikuingilie kwa njia ya kisasi....hivyo utafikiri unalipiza kisasi kumbe ndio unathibitisha miunganiko ambayo awali hukuwa nayo.!
Kitacho tokea hapo
Mwanaume ataendelea kujiunganisha na minyororo mibovu na mwanamke hataacha kutoboka
Maana tayari mnyoro wenye dhiki nyingi...
Kiufupi ndoa inakufa na kuchakaa kabisa....

BINTI : tunza utu wako(nafsi)yako ni ya thamani Sana kuliko chochote
Na ndio vishawishi ni vingi Sana kwajili ya kuangamiza nafsi yako.

KIJANA : Tunza utu wako wa ndani ni gharama sana kuja kuurekebisha ikitokea umeupeleka utumwani...

HILI SOMO LIISHIE HAPA KWA LEO
Litaendelea.........

Content created by : CREEZLE FAREY
 
Kifua cha kahaba kimebeba laana na mikosi.
U..ke ni kaburi la kuzimu
 
Back
Top Bottom