Aliyewahi kutapeliwa kwa kuuziwa dawa feki za kienyeji atoe ushuhuda

Aliyewahi kutapeliwa kwa kuuziwa dawa feki za kienyeji atoe ushuhuda

James Kasonda

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
84
Reaction score
49
Watu wengi sana wamewahi kutapeliwa kwa kuuziwa dawa feki za kienyeji kwa gharama kubwa lakini wanalalamikia chini-chini. Kwa kuwa huwa tunajifunza kwa makosa, naomba mtu yeyote aliyewahi kutapeliwa ajitokeze humu janvini kwa faida ya jamii nzima ya Tanzania. Jamani tuungane tuwe kitu kimoja katika kupiga vita utapeli unaozidi kushamiri nchini kwa kasi kubwa. Sio lazima utaje jina la mganga, sema tu ulitapeliwa dawa ya kutibu nini, kama hilo pia ni gumu sema tu mahali ulipotapeliwa mfano: Dar au Songea, Iringa nk. Naanza mimi.
1. Niliuziwa dawa feki ya kushinda mashindano ya mbio Iringa
2. ...
 
James Kasonda naona una bifu na akina tambalamiti
  • Kutapeliwa inatoka wapi hapa tena wakati unakuwa umekubaliana na mteja wako;

  • Hata babu wa loliondo alisema ni imani yako ndo itakuponya.
 
Last edited by a moderator:
James Kasonda naona una bifu na akina tambalamiti
  • Kutapeliwa inatoka wapi hapa tena wakati unakuwa umekubaliana na mteja wako;

  • Hata babu wa loliondo alisema ni imani yako ndo itakuponya.

Yah naona ana bifu tu na mtu humu, kutapeliwa atapeliwe yeye huko Iringa kwa kushindwa kukimbiza upepo halafu atake watu watoe ushuhuda JF? Kazi tunayo.
 
nishatapeliwa mara nyingi dawa za kuongeza uume na kunenepesha yaani hata mara kumi inafika.
na sijawahi kuona mabadiliko .
mara ya kwanza nilisoma tangazo kwenye gazeti nikatuma hela dar 30,000 wakatuma dawa ikawa hola.
mara ya pili ubungo walikuwa na gari kabisa watu kibao wakawa wana nunua na mimi ikanitoka 10,000.
hizo mara zingine huku mikoani.
yaani sasa hivi sitaki hata kusikia hao matapeli
 
naona una bifu na akina tambalamit
[*]Kutapeliwa inatoka wapi hapa tena wakati unakuwa umekubaliana na mteja wako.

Jaman hodi! kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
Mi nafikiri mtoa hoja anamaana nzuri tu ya kutusaidia na sie wengine tusipigwe.
Ila neno alilotumia ndo laweza kuleta mkanganyiko.
Hii imekaaje "Kwa wale ambao wamewahi kutumia tiba mbadala ambazo ni maarufu kwa sasa je wamewahi kufanikiwa malengo
yao?. Hapa wakina Dr. Tiba mbadala, na Maprofessor wanahusika.
 
Back
Top Bottom