peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 18,223
- 31,465
Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (RPC), SACP Absalom Mwakyoma, amefariki dunia leo Jumatatu, Aprili 7, 2025, baada ya kuugua ghafla.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa SACP Mwakyoma alifariki dunia saa mbili asubuhi akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya KCMC kutoka nyumbani kwake eneo la Shule ya Msingi JK Nyerere, Manispaa ya Moshi.
SACP Mwakyoma alihudumu katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Pwani, Kilimanjaro na Mara, na alistaafu Januari mosi, 2013, akiwa RPC wa Mara.
Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya KCMC na unatarajiwa kusafirishwa kwenda Mbeya kwa maziko baada ya taratibu kukamilika.