TANZIA Aliyewahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, John Mwanga afariki dunia usiku wa kuamkia leo

TANZIA Aliyewahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, John Mwanga afariki dunia usiku wa kuamkia leo

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mwanasiasa John Mwanga (78), aliyewahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Machi 5, 2025.

Mwanga, ambaye aliweka historia kuwa mbunge wa kwanza wa Moshi Mjini baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini, amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Selian, mkoani Arusha, ambako alikuwa akipatiwa matibabu kutokana na kuugua kwa muda mrefu.

mbunge john.png

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na mtoto wake, Fortunate Mwanga, ambaye ameeleza kuwa baba yake alikuwa akiugua kwa muda mrefu.

"Ni kweli baba yetu amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Selian, ambapo alikuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu," amesema Fortunate.

Amesema taratibu za mazishi zinaendelea na zitafanyika mkoani Arusha, Dar es Salaam na nyumbani kwake, Usharika wa Neema, KCMC, mkoani Kilimanjaro.

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom