TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

R.I.P mkuu wa mkoa wa dar mstaafu, hivi kwa nini viongozi wazuri huwa wanakufa mapema wabovu wanabaki?
Iyo ni kazi ya Mwenyezi Mungu,Mwenye kujua huyu mwema ama muovu ni yeye Mwenyezi Mungu na sio sisi
 
Huyu jamaa alikuwa na busara sana!!! nakumbuka akiwa mkuu wa Wilaya Singida alivyotatua mgogoro wa mgomo pale Mwenge secondary baada ya kifo cha mwanafunzi Chresencia Tarimo. R.I.P baba husna R.I.P Cresencia Tarimo
 
Rest in peace, Tutakukumbuka kupitia maji ya kufunga kwenye mifuko,Maji ya Kandoro
 
R.I.P mzee kandoro. Ila kuna la kujifunza hapa Kwa huyu mzee, yaani ccm wengine wakifa page ya kwanza huwa inajaaga washangiliaji Kwa huyu mzee imekuwa tofauti viongozi wengine wa ccm jipangeni
Kandoro hakuwaga na majivuno wala siasa taka
 
Ilikuaje yakaitwa jina lake ?
Alikua ni mkuu wa mkoa aliyepinga vikali maji ya kwenye plastic bag. Ilikua ni katika kupambana na uchafuzi wa mazingira. Kipindi hicho hayo maji yaliuzika sana kabla ya mkuu huyo wa mkoa kukataza
 
Back
Top Bottom