TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

Imethibitishwa Abass Kandoro hatunaye tena. Source inasema alikuwa ICU kwa muda mrefu sana.

Kandoro amewahi kuwa katika nafasi ya ukuu wa Mkoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipomtembelea Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Aprili 25, 2018.
Msiba huu uwakumbushe walioko madarakani na kijifanya miungu kuwa yote ni ubatili mtupu kuna siku nao mauti itawakuata
 
Alikua mkuu wa mkoa katili sana alivunja vibanda vya wamachinga mji mzima, nakuzuia uuzwaji Maji ya mifuko ndipo lilipo toka jina Maji ya kandoro, hakuwa mtu mzuri tuache unafiki
 
Pamoja na mapungufu kidogo hasa kwa ajili ya uCCM lakini alikuwa anajitambua, busara kama za akina Meck sio huyu mwizi wa cheti mkurukupukaji.RIP kiongozi.

Kwa uchache, namkumbuka kama mtu aliyekuwa na haiba ya uongozi, alijaa busara na alijua kutumia kinywa chake. Namkumbuka pia kwa kufanya vizuri kwenye usuluhishi wa migogoro mbalimbali ya kijamii.
 
RIP Kandoro.Ndio utajua kifo hakina mwenyewe.Kuna MaRC wanajifanya Mungu mtu kumbe mwisho wa siku six feet under
 
Msiba huu uwakumbushe walioko madarakani na kijifanya miungu kuwa yote ni ubatili mtupu kuna siku nao mauti itawakuata

Ni maoni ya ajabu, yasiyo na utu kabisa...kifo ni kwa yeyote yule hata wewe unayeleta kejeli kwa kifo cha wenzio nawe utakufa
 
Mungu in noma hajui kama ulikuwa kwenye dola wala mini,kamchota.muwakumbushe na wengine kwamba kifo ndio kiboko cha mwanadamu.
 
Ni maoni ya ajabu, yasiyo na utu kabisa...kifo ni kwa yeyote yule hata wewe unayeleta kejeli kwa kifo cha wenzio nawe utakufa
siwezi kujisahau kwani natabua hilo ila walevi wa madaraka hujisahau
 
Back
Top Bottom