Aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya apigwa marufuku kuingia Marekani kwa madai ya rushwa

Aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya apigwa marufuku kuingia Marekani kwa madai ya rushwa

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Hii inawezekanaje nchi yenyewe iliyofanyiwa huu unyama wa rushwa haishituki wala kuchukua hatua yoyote badala yake wazungu ndiyo wanaochukua hatua?, au ndio ile hadithi ya " mwisi yetu?". Msipoangalia hata Uhuru Kenyatta akimaliza muda wake atapigwa marufuku.

====
Marekani imemweka aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya Amos Wako katika orodha ya watu waliopigwa marufuku kuingia Marekani kwa madai ya kuhusika katika rushwa.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Voice Of America, Kulingana na taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Wako, pamoja na mkewe Flora Ngaira na mwanawe Julius Wako, wamepigwa marufuku kuingia Marekani.

Serikali ya Marekani inasema hatua hiyo imechukuliwa kutuma ujumbe kwamba Marekani inashirikiana na Kenya katika kupambana na rushwa.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaelezea waziwazi ni vitendo gani vya rushwa Wako alihusika navyo.

Wako alikuwa mwanasheria mkuu wa Kenya kwa muda wa miaka 20, kati ya mwaka 1991 na 2011.

Amos Wako kwa sasa ni seneta wa Kaunti ya Busia, magharibi mwa Kenya na vyombo vya habari vya Kenya vimemhusisha na nia ya kutaka kugombea nafasi ya gavana katika Kaunti hiyo.

Chanzo: VoA Kiswahili
 
Amos Wako ni janga tangu zamani. Afadhali US wameliona hilo.
 
Wapigwe marufuku kabisa, hakuna Mkenya ambaye ana hamu na hawa wanasiasa mafisadi. Ila mleta mada nawe pia ni jipu. Kwenye taarifa hiyo ambayo umeipost wewe mwenyewe wamarekani wenyewe wanasema kwamba wamechukua hatua hiyo kwasababu nchi za Kenya na Marekani zinashirikiana pakubwa kwenye vita dhidi ya ufisadi. Hata Kiswahili pia kinakukanganya?
 
Wapigwe marufuku kabisa, hakuna mkenya ambaye ana hamu na hawa wanasiasa mafisadi. Ila mleta mada nawe pia ni jipu. Kwenye taarifa hiyo ambayo umeipost wewe mwenyewe wamarekani wenyewe wanasema kwamba wamechukua hatua hiyo kwasababu nchi za Kenya na Marekani zinashirikiana pakubwa kwenye vita dhidi ya ufisadi. Hata kiswahili pia kinakukanganya?
Kama hapo Kenya hamjamkamata wala kumshitaki mahakamani, mumemwacha anatembea akiwa huru, huo ushirikiano wenu ni upi?. Jambo la kushangaza ni kwamba huyu jamaa ufisadi ameifanyia serikali ya Kenya, kweli GoK imeshindwa kumshughulikia hadi ishirikiane na Marekani?. Mbona ni jambo dogo sana linaloweza kufanywa na serikali ya Kenya?. Tatizo lenu serikali yenu imekatwa na wenye pesa, hamna uwezo wa kuwagusa.
 
Tunashangaa Sana vile 1.5 trillion yenu hakuna aliyeshtakiwa.
 
Tunashangaa Sana vile 1.5 trillion yenu hakuna aliyeshtakiwa.
Mbona huyo "Mungu" wenu asione huo ufisadi wa hiyo trilioni 1.5 na kuwawekea vikwazo walio husika badala yake ninyi vibaraka wake ndio anawawekea vikwazo?. Vipi Tanzania ichaguliwe kuwa ndio nchi namba moja Afrika ktk kupambana na rushwa na ufisadi kama kungepotea pesa nyingi kiasi hicho?
 
Still waiting for your response to the 1.5 trillion shilling corruption scandal.
 
Wajinga ninyi, hadi nchi za nje zimeamua kuwasaidia kupambana na mafisadi wenu, ninyi wenyewe mnachekacheka tu, Failed state.
Ila kama vile namuonea huruma Mr Wako ukiangalia the role he has played to save Kenya from total collapse post PEV!
 
Wamarekani ndio waliiba hio 1.5 trillion yenu vile Barrick wanavyopora dhahabu yenu?
Hakuna 1.5trillion iliyoibiwa, ni vile Kuna a lot of procurement zilifanyika ambazo hazikukaguliwa na cag, like the planes, railways, relocation to Dom etc.

1.5trillion is a lot of money kuibiwa tu namna hiyo.
 
Ila kama vile namuonea huruma Mr Wako ukiangalia the role he has played to save Kenya from total collapse post PEV!
Aliplay role gani? Hatuna huruma na wafisadi. Wakatwe vichwa vitupwe kwa choo.
 
Aliplay role gani? Hatuna huruma na wafisadi. Wakatwe vichwa vitupwe kwa choo.
Mbona ninyi wenyewe hamumkamati, badala yake mnazidi kumshirikisha ktk mambo mbalimbali ya kitaifa?.
 
Back
Top Bottom