UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Unaona namtetea kwa sababu ninyi kwa kuongozwa na hisia za chuki mmekuwa kama mmeweukwa linapokuja suala la Magufuli. Mnataka kutuaminisha kwamba Tanzania ilikuwa shwari hakuna kutekana, kutesana na kuuwana ila hadi alipoingia Magufuli wakati akina Dr. Ulimboka walitekwa na kuteswa kwa nia ya kuuliwa ila siku zake hazikufika kama Lissu, huko Zanzibar washauliwa sana watu hadi watu wakapakimbia, wapinzani washapitia mateso sana tu huko nyuma washapigwa hadi mabomu watu wakafa kuna watu hadi leo ni walemavu kabisa, hao polisi washatesa na kuuwa sana raia huko nyuma. Walikuwepo akina Mtikila na wakanyamazishwa.Utamtetea sana huyo muuaji lakini Mungu ameshapitisha hukumu yake na wote wapenda haki na amani tumefurahi
Sasa tukiongea haya tunaonekana tunamtetea Magufuli kwamba hamtaki kuyasikia hayo bali nyie mnataka wote tuungane kumchukia Magufuli na kuaminishana kwamba Tanzania ilikuwa shwari kila kitu ila tatizo Magufuli alikuja kuharibu kila kitu, imefika hatua hadi leo Kikwete na Kinana wanaonekana ni watu wema(sijajua wema huo ni hadi mbele za Mungu au kwa binaadamu tu?) na ndio maana hawajafa wako hai.