TANZIA Aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Jaji wa Mahakama Kuu na Mbunge wa Ifakara, Edward Anthony Mwesimo afariki dunia

TANZIA Aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Jaji wa Mahakama Kuu na Mbunge wa Ifakara, Edward Anthony Mwesimo afariki dunia

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Moja kati ya manguli ambaye amehudumu katika mihimili yote ya dola, amepumzika. Ni Mh. Jaji Mstaafu Edward Anthony Mwesiumo.

Alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, katika nafasi hiyo aliwahi "kukwaruzana" na Mwalimu Nyerere baada ya kukataa "maelekezo" kuhusu jalada nyeti lililokuwa mbele yake.

Baada ya dola kugundua amekataa maelekezo, asubuhi akakuta ofisi yake imesachiwa na jalada halipo. Kwa kuwa alikuwa analijua jalada, mwamba akapiga jajment kwa kutumia facts alizokuwa nazo kichwani. Halafu akasoma hukumu. Dola ikachachamaa, ikamuondoa Mahakamani kwa "mizengwe"

Mpaka siku za karibuni, amekuwa akiandika barua ikulu akiomba alipwe mafao yake ya Ujaji, lakini wapi.

Kwa Mwesiumo haikuisha mpaka iishe, akagombea ubunge huko kwao Morogoro, akachanua kama maua rose, akashinda kwa kishindo. Mzee Mwinyi akampa wizara ya mambo ya ndani, akiwa Naibu Waziri, Waziri Mrema.

Mambo yakaenda yalivyoenda, nadhani bado mambo yalikuwa hayajaisha,Dola ikaendelea kumchimba, nadhani dola ilimpachika kajambo, u waziri ukaondoka, na ubunge akaukosa. Akachoma mahindi sana.

Alikuwa Mwalimu Tumaini university Iringa, Jaji Ramadhani akatembelea Chuo, akamkuta huko, akafamfanyia maarifa, Mwesiumo akateuliwa kuwa Kamishna katika Tume ya kurekebisha sheria Tanzania.

Nadhani Mahakama, Bunge na serikali zimtendee haki kwa kumpa heshima yake. Sijaona Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wala taasisi ya umma ikitoa salamu za pole.Na ninadhani hata msiba hawatahudhuria. Moja kati ya waoiofanya kazi na marehemu, ni Prof Juma.

Screenshot_20241120-073432.jpg
 
Another proof hii ni nchi ya "kijamaa" typical..


Pumzika kwa amani mzee wetu.
 
R.i.P Classmate....😥
Jaji aliekua na misimamo yake....😊
Ila hii nchi bila unafiq, utaundiwa zengwe tu...🤨
 
Utawala wa nyerere nao uliingilia uhuru wa mahakama. Kumbe hii tabia ilianza muda mrefu
 
Back
Top Bottom