GE2025 Aliyoyaahidi Yeriko Nyerere kwenye kampeni za mtaa kwa mtaa kusaka kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Yericko Nyerere, amefanya kampeni za aina ya kipekee alizozitaja kuwa “Mobile Campaign”, akiwafuata wananchi walipo na kuhutubia mikutano ya hadhara akiwa njiani bila kutumia jukwaa rasmi, huku akipata mwitikio mkubwa wa mamia ya wakazi wa Kigamboni.

Mikutano hiyo imefanyika katika maeneo ya Feri Standi, Mwasonga Stendi na Kisarawe II, ambapo licha ya mvua kubwa kunyesha katika baadhi ya maeneo, Yericko ameendelea na kampeni akisisitiza dhamira yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia vipaumbele vinne vya msingi.

Soma pia: Yeriko Nyerere nadi sera za CHAUMMA achana CHADEMA

1760008881035.png

Mikutano hiyo imeongozwa na Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo, Mheshimiwa Salum Mwalimu, ambaye pia amekuwa akitumia mtindo wa kampeni za “mtaa kwa mtaa” katika maeneo mbalimbali.
Yericko amesema kipaumbele chake cha kwanza ni kuboresha miundombinu ya barabara zote za Kigamboni kwa kuhakikisha zinajengwa kwa kiwango cha lami.

Ameeleza kuwa atatumia nafasi yake bungeni kuishawishi Serikali Kuu kutenga bajeti maalumu ya ujenzi wa barabara za Wilaya na mitaa, huku pia akipendekeza bajeti ya Halmashauri iongezwe mara kumi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara kuu kutoka Feri hadi Pembamnazi na kutoka Ndundwi Songani hadi Feri.

Kipaumbele cha pili kwa Yericko ni kuondoa tozo za daraja na vivuko, akizitaja kuwa mzigo usio wa haki kwa wananchi. Amesema deni linalotajwa na Serikali kuhusu mradi wa Daraja la Kigamboni kuwa ni la NSSF halina msingi wa kiuchumi, na kwamba akichaguliwa, atashauri Serikali Kuu kubeba deni hilo na kuongeza ruzuku za uendeshaji wa vivuko.

Amebainisha kuwa fedha za kugharamia hatua hizo zinaweza kupatikana kutokana na ongezeko la mapato ya Bandari ya Dar es Salaam baada ya uwekezaji wa kampuni ya DP World, ambapo mapato yamekuwa yakiongezeka kwa wastani wa shilingi trilioni 1.8 kila nusu mwaka.

Yericko pia amegusia changamoto ya maji, akisema ni tatizo sugu lililodumu tangu uhuru wa nchi. Ameeleza kuwa, licha ya Kigamboni kuwa na visima vikubwa vinavyotoa maji yanayohudumia maeneo ya Posta, Mbezi na Masaki, wakazi wa Kigamboni wenyewe wameendelea kukosa maji safi na salama.
Ameahidi kwamba, endapo atachaguliwa, atatenga siku 60
 
View attachment 3486075

20251009_110439.jpg
 
Back
Top Bottom