USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 12,213
- 28,916
Anaandika Mwl. Mbelwa Petro.
ALIYOYAFANYA DAKTA SAMIA SULUHU NA MBUNGE EZRA JOHN KWA AJILI YA BIHARAMULO NA TANZANIA, ACHA SIASA IWE UPENDO.
Tangu serikali ya awamu ya sita chini Rais Dakta Mama Samia ianze kazi, wilaya ya Biharamulo tumenufaika na miradi mingi iliyogusa maeneo yote muhimu ukilinganisha na awamu nyingine zilizopita kibajeti.
Falsafa zake za maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upya, Mama Samia amedumisha utu wa watu anaowaongoza kila kona ya nchi.
Kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo siku ya Jumatano ya 28 Octoba, mwaka 2020 nikiwa mgombea wa kiti cha ubunge kupitia CHADEMA kwenye Jimbo la Biharamulo huku Ezra akiwa mgombea wa CCM, pasipo kujua nilikuwa nashindana na mtu ambaye, chini ya catalysing ya uzalendo na mapenzi ya Rais Mama Samia Suluhu amekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa wakati wake ametizamwa, akapimwa na akatosha kuwa:
1. Rais wa Kamati ya kudumu ya masuala ya kibinadamu na kijamii katika nchi za eneo la maziwa makuu i.e DRC, Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan ya kusini, Uganda na Kenya.
2. Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
3. Kiongozi wa timu ya kampeni ya kuhakikisha Mheshimiwa Tulia Ackson, Spika wa Bunge la JMT anashinda kwa kishindo Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika nchini Angola akiwazabua Catherine Gotani Hara wa Malawi, Adji Diarra Kanouté wa Senegal na Marwa Abdibashir Hagi wa Somalia. Tulia Ackson akawa mwanamke wa kwanza kuongoza bunge hilo lenye nchi wanachama 179 na wabunge 705 wanaoziwakilisha nchi zao, akichukua nafasi ya Duarte Pacheco Spika wa Bunge la Ureno, ambaye alichaguliwa mwaka 2020.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
4. Ameuliza maswali 65 na akatoa michango mara 45 katika Bunge la JMT kwa kipindi cha 2020-25 kabla ya kikao cha mwisho cha Bunge hilo. Idadi ya maswali na michango mingi zaidi ukiilinganisha na wabunge wengine.
5. Na kwa ufupi sana, mbunge ambaye "amemoka" na kupitia "kumoka" kwake Constituency Development Catalyst Fund" (CDCF) yaani "Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo", fedha yake imeongezwa kutoka 69,000,000T mwaka 2021/22 na kuwa milioni 92,000,000T kuanzia 2022/23 {Na kazi zake zimeonekana}.
6. Amefanya tireless advocacy kuhakikisha bajeti ya miundombinu ya barabara za Jimbo letu la Biharamulo zinaongezwa kutoka milioni 670,000,000T mpaka 2,467,000,000T.
7. Mbunge ambaye amekuwa chagizo la ongezeko la Zahanati 26 kutoka Zahanati 18, vituo vya afya kutoka vituo 6 mpaka 7, kimoja wapo kikiwa ni kituo cha Afya cha Bisibo ambacho kimeigharimu serikali ya Mama Samia kiasi cha 500,000,000T huku Hospitali ya serikali ya Wilaya ikiwa ikiwa imeshagharimu 2,580,000,000T mpaka sasa.
8. Ongezeko la shule za misingi kutoka shule 98 mpaka shule za misingi 119.
9. Ongezeko la shule za sekondari kutoka shule za sekondari 18 mpaka shule za sekondari 28. Mojawapo ikiwa ni shule ya sekondari Kabhulaisoke ambayo imeishagharimu serikali ya awamu ya sita kiasi cha 584,280,029T.
10. Kati ya mwaka 2020 mpaka 2024 capitation grants iliyokuja wilaya yetu ya Biharamulo kwa ajili ya kugharamia elimu ya sekondari bila malipo ni 3,761,056,746.61T, hii ni sawa na kilo 376.1 za pesa, noti moja ya 10,000 na uzito wake wa gramu moja.
11. Biharamulo tumepokea kiasi cha 1,313,753,952T kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo kwa shule za msingi.
12. Ujenzi wa maegesho ya magari makubwa Nyakanazi tumepokea kiasi cha 3,371,101,542T.
13. 8,800,000,000T zimekuja Biharamulo kwa mara ya kwanza tangu zama za Adam na Eva kuhakikisha upatikanaji wa huduma za maji safi, salama na ya kutosha katika vijiji vyetu ambapo:
a) Mradi wa Maji Kabindi ambao umewagusa wananchi wa maeneo ya Rukora, Chebitoke, Kikomakoma na Kabindi.
b) Mradi wa maji Runazi ambao utawagua wananchi wa maeneo ya kijiji cha Runazi na Migango.
c) Mradi wa maji Kabukome ambao utawagusa wananchi wa Kabhukome.
d) Mradi wa maji Nyantakara, mradi utakao wagusa wananchi wa kijiji cha Nyantakara.
e) Mradi wa maji Nyakahura awamu ya I, mradi utakaowagusa wananchi wa vijiji vya Nyakahura, Ngararambe, Rugese, Mihongora na Mabale.
f) Mradi wa maji Nyamigogo-Songambele, mradi huu utawagusa moja kwa moja wananchi wa vijiji vya Nyamigogo, Songambele na Kagoma.
g) Mradi wa maji Busiri-Midaho utakao wagusa wananchi wa Kikoma na Busiri.
h) Mradi wa maji Nyabusozi-Mbindi utakaowagusa wananchi wa Nyabusozi, Mbindi na Mwanga. Na miradi mingine kama hiyo katika maeneo ya Kasilo, Nemba, Mavota, Mbaba, Nyamigere, Kalenge, Katahoka, Ruganzu, Ntumagu, Rusenga, Nyamalagalla na Nyambale.
14. Juhudi kubwa za serikali ya Mama Samia tayari zimeshagharamia jumla ya 3,302,862,402T katika kuhakikisha mtandao wa maji mjini unaongezeka, ambapo maunganisho mapya ya maji yamefikia 5,750 kufikia Januari 2025, kutoka wateja 2164 mnamo mwaka 2020.
15. Nishati ya umeme kwa Mwaka 2020: umeme ulikuwa umefikia senta 46 tu za vijiji vyetu Biharamulo, leo umeme umesukumwa na kusimikwa kwenye senta za vijiji vyote 74. Tumebaki na kazi ya kufikisha vitongojini mwetu. Ndiyo maana CHADEMA hawataki kushiriki uchaguzi huu 😆😆.
16. Mwaka 2020 wakati nasigana na mbunge huyu kulikuwa na maunganisho ya mita za umeme 13,305 tu, kufikia Machi, 2025 wilaya yetu ilikuwa na jumla ya maunganisho ya mita za umeme 19,949 zikiwemo taasisi za shule, vituo vya afya, Zahanati na maghala ya mazao yetu.
Nahitaji nini kuendelea kutoamini juhudi za Rais Mama Samia huku naona mambo yaliyokuwa hayawezekani sasa yaawezekana?
Nifanye ligi na Mbunge Ezra kwa kumuona hawezi kufanya uchechemuzi kwenye eneo lipi tena?
Mahali alipofika Mbunge Ezra John anahitaji kuonyeshwa upendo, na ndio maana tunasema SIASA NI UPENDO.
Sijafikiria na sihitaji kufikiria tena kushindana kisiasa (kugombea) kwa sasa, ni wakati wa kushikamana na viongozi wetu waliopo sasa na watakaokuja kuhakikisha tunawalinda na kulinda kile wanachokifaya kwa ustawi wa vizazi vyetu, hiyo inatosha.
Kwa juhudi za ki-vitendo za Dakta Mama Samia katika kuleta Mageuzi {reforms}, Maridhiano {Re-conciliation}, Ustahimilivu {resilience}, na Kujenga upya {re-build} mifumo ya nchi yetu, ni wakati wa kuiishi kauli mbiu ya KAZI NA UTU - TUNASONGA MBELE. Mama Samia kupitia Falsafa 4R ameponya na kudumisha ki-vitendo urithi tulioachiwa na Wazee wetu, akina Julius Kambarage Nyerere, Mzee Abeid Karume, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Tewa Said Tewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela-Bantu, John Rupia, Abdul Wahid Sykes n.k ambao walihangaika mno kuileta Tanzania salama, yenye amani, yenye Maendeleo na moja.
Mwl. Mbelwa Petro,
Singida,
0759886429.