Uchaguzi 2020 Aliyoyatamka kwenye kampeni yote yametimia, kwanini asiapishwe?

Uchaguzi 2020 Aliyoyatamka kwenye kampeni yote yametimia, kwanini asiapishwe?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wakati wa kampeni Magufuli alisikika akisema, nileteeni diwani na mbunge wa CCM, alikua na uhakika wa ushindi wake. Yale aliyosema yote yametimia. Majimbo karibu yote ya Tanzania yame pata diwani, mbunge na Magufuli wa CCM.

Ni kwanini tupate tabu tena kuhangaika na uchaguzi 2025. Hizi pesa tunazopoteza kwenye uchaguzi ilhali Magufuli anachosema kinakua si kheri zisaidie ujenzi wa barabara za lami vijijini na maji salama ya kunywa.

Pangeni sherehe ya kumuapisha Magufuli awe Mfalme wetu. Tutekeleze kauli zake kwani tume fanya hivyo kwa miaka mitano. Ata pata nafasi ya kuteua anaowapenda wamsaidie kuuongoza ufalme wake.

Kipigo walichopata raia wasio na silaha waliojaribu tu kuandamana ili kupaza sauti ya uchaguzi usio na haki, kinatosha kutufahamisha kuwa tunatakiwa kuiabudu CCM. Ukihoji maagizo kutoka juu imekula kwako.
1604055275260.png
 
Tunakoelekea ukiwa na kadi ya Chadema utakua mhaini wa Ufalme.
Usiwe na wasiwasi; maisha yataendelea kama kawaida; asiyekubali kushindwa siyo mshindani. Mimi nlianza na kadi ya TANU Youth League mwaka 1973, halafu baadaye nikapata kati ya CCM mwaka 1978, na baadaye nikapata kadi NCCR-Mageuzi mwaka 1995 baadaye nikapata kadi ya CHADEMA 2009. Kadi zote hizo bado ninazo na wala siyo mfuasi wa chama chochote tena na maisha yanaendelea tu.
 
Yaani Nyie Ni Vilaza kweli
Kwa Akili yenu Mliamini Huyo Mamluki Amshinde Magufuli kweli
Kutwa na Vi ID vyenu uchwara kumi kumi humu Na Kelele kama vitoto vya Ndege kwenye Kiota
Tuliwaambia Mkipata 20% mjue mmeshinda
Ahahaha baambie baelewe
 
Usiwe na wasiwasi; maisha yataendelea kama kawaida; asiyekubali kushindwa siyo mshindani. Mimi nlianza na kadi ya TANU Youth League mwaka 1973, halafu baadaye nikapata kati ya CCM mwaka 1978, na baadaye nikapata kadi NCCR-Mageuzi mwaka 1995 baadaye nikapata kadi ya CHADEMA 2009. Kadi zote hizo bado ninazo na wala siyo mfuasi wa chama chochote tena na maisha yanaendelea tu.
My friend don't be that cheap, it is our Children and our lives, and we live only once!
 
Kama ilivyokuwa kule Zanzibar, ukiwa na kadi ya chama cha upinzani wewe ni adui. Huenda itabadilika sasa.
Zenji sasa upinzani ni uhaini rasmi, kama tujavyosikia ni kweli kuwa Jusa yu taabani basi tujue wako wanaofuatwa majumbani kama si kutishwa basi kuoneshwa "sasa mnasemaje!?" Chema dunia imeona.
 
Back
Top Bottom