Kumekuwepo na malalamiko kuwa wanawake - (wake na ma GFs) wanamegwa sana siku hizi na wanaolalamika hawajakaa wakajiuliza hivi kwanini inakuwa hivi.
Moja ya sababu za kuleta hali hii inayowasumbua na kuwaumizi mioyo wahusika ni vijitabia hivi vya kuzungukanazungukana.Wewe wako unataka abakie wako, ila wa wenzio ni halali yako - nini unadhani kitakufanya wewe uwe so special kiasi kuwa wenzio wanaokuona ukimendea vyao wakuachie vyako?...
Katika utafiti wangu mdogo niliowahi kuufanya kuhusu ishu hii nimepata kuwa wanawake wenye watu wao mara nyingi hawapendi ( nasema tena MARA NYINGI sio MARA ZOTE) kuwa na mahusiano ya ziada au ya pembeni kwa sababu wanaridhika wako tayari na mahusiano.
Wale wanawake wanaojihusisha na mahusiano ya pembeni hufanya hivyo kwa sababu mbalimbali - kuna ambao ni hulka, wako ambao wanakosa mapenzi kwa waume/boyfriends, wako ambao hurubuniwa kirahisi kwa kuwekwa katika hali hatarishi (compromising situations) na kuingia kwenye mtego bila kutarajia.Moja wapo ya gia wanayorubuniwa nayo hao akina dada/mama na hao wapenzi wa nje ni kupewa data kamili zinazohusu waume/BFs wao na hata mara nyingi kwa ushahidi kamili wa maneno yanayozungumzwa, picha za matukio etc.Hi hupelekea kuchochea hisia za kulipiza kisasi.
Najua kuna watakaopinga na kubisha lakini habari ndio hiyo.