Ally Bananga: Mwizi karudisha vitu vyetu halafu analazimisha tumsifu

Ally Bananga: Mwizi karudisha vitu vyetu halafu analazimisha tumsifu

Mkuu hii ni awamu nyingine Mkuu wangu. Msitumie title ya 'mwizi' mambo yamebadilika sana...
Awamu hii ni tofauti na zilizopita, mnaposema amerudisha mmenifurahisha.

Mnaamini katika mabadiliko, mabadiliko ndio haya sasa. Wananchi wameyapata mabadiliko humohumo ndani ya CCM... Mkuu kuna mabadiliko makubwa sana unless unatumia miwani ya kiitikadi.

Mkuu mambo sahivi yanapendeza, kunanoga Mkuu.

La mwisho jiulize, kama huyu unayemuita 'MWIZI' maweza kurudisha kilichoibiwa kwa miaka 50+ ndani ya awamu moja yenye miaka 5 tuu je akimalizia na mitano mingine huoni tutapiga hatua za miaka 50+ mbele?

Haya je tukiamua kufuata na ushauri wa mzee Mwinyi je[emoji23][emoji23]... (nisitoke nje ya mada).

JPM[emoji106][emoji106]

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
MWIZI KARUDISHA VITU VYETU ALAFU ANALAZIMISHA TUMSIFU"
 
Muuaji hawezi kupata kura yangu!
 
KAULI YA BANANGA INATISHA; "MWIZI KARUDISHA VITU VYETU ALAFU ANALAZIMISHA TUMSIFU"​

Na, Robert Heriel

Moja ya watu waliotisha siku ya jana kwenye mkutano wa Kampeni wa CHADEMA huko Tabata Segerea ni pamoja Ally Bananga. Sikuwahi kumjua huyu Bananga, siku ya jana ndio nimemuona na kumsikia. Hakika huyu ni mtu muhimu sana kwa CHADEMA kwa wakati huu. CHADEMA mchukueni huyu mtu, angalau apewe Dakika kumi au kumi na tano kabla ya saa kumi na moja.

Kauli zote za Bananga ni muhimu, Kauli zote za Bananga zinashtua ubongo uliolala. Kauli zote za Bananga zinahamasisha, zinachangamsha, zinatia uchungu, na pia zinamfanya msikilizaji achukue hatua.

Bananga kila alichoongea kiliingia katika akili ya aliyekisikia. Ni watu wachache kama Bananga wenye uwezo wa kuwasilisha hoja kwa namna yake.

Kwa Mujibu wa Bananga, ameomba Muongozo kwa Mgombea wake wa Urais, kisha na wasikilizaji waliokuwa wakimsikia kuwa; Mwizi karudisha vitu alivyotuibia, alafu analazimisha tumsifu, hiyo imekaaje.

Bananga anajaribu kuzishtua akili za wasikilizaji kuwa, Mambo mengi ambayo CCM wameyasema wameyafanya yalikuwepo, ametoa mfano wa ndege, treni na reli,

Bananga anasema, mambo hayo yalikuwepo lakini yaliuawa na haohao CCM, kisha leo wanarudisha vitu vilivyokuwepo wanajisifu. Hiyo imekaaje.

Kuhusu Ndege sikuwepo, lakini Treni ya kaskazini nilikuwepo kipindi ikiwa inafanya kazi zake. Baadaye Treni ile iendayo Moshi ilikufa chini ya utawala uliowekwa na CCM. Sasa kitendo cha Serikali ya awamu hii chini ya CCM kusema imeleta maendeleo katika ufufuaji wa Reli iliyokufa chini ya utawala wao huohuo wa CCM, ni mfano wa mwizi kukurudishia kitu alichokuibia kisha akalazimisha umsifu.

Hii ni kama muda huu ambapo serikali ya awamu hii imesitisha nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa serikalini alafu baadaye serikali hiyo hiyo iongeze mishahara ambayo yenyewe ilisitisha nyongeza alafu ilazimishe kusifiwa.

Ni sawa na mtu anayekupiga kofi kisha anakubembeleza kisha anajisifu kwa kukubembeleza.

Au ni sawa na mtoto umchape kisha umpe pipi ya kumrubuni ili anyamaze.

Au ni sawa na Mwizi kakuibia Gari Kisha anakurudishia akiwa kalipaka rangi muda huo umechapika. Alafu anajisifu nimelipaka rangi, hasemi yeye ni mwizi wala haombi samahani kwa kukuibia hamna yeye anajisifu kakurudishia gari lako.

Ally Bananga apewe Dakika 10 hadi 15 kuongea, anaweza kuwafikisha CHADEMA Somewhere. Jamaa anajua kuongea, anajua kuhamasisha.

Nashukuru CHADEMA kwa kuweza kufuata baadhi ya ushauri wangu wa namna ya kuwasilisha hoja zenu Jukwaani. Kule Segerea Mlifanya vizuri kwa 80%.

Tafuteni kama kina BANANGA 3

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Bananga ni sawa na msalani tu
 
Chadema walipomtema Slaa ilijulikana tu kuwa wako kwa ajili ya hela, walianza kukumbatia ufisadi, sasa hivi wako na Wazungu waliokuwa waibe Madini yetu.
Nahisi wakikamata lazima nchi hii watumbukize kwenye kesi waktadaiwa tulikiwa na kesi sasa tunalipa.
Swala la MIGA sijawahi kusikia mgombea amelimalizaje la kushtakiwa.
Bora nijaribishe kwa CHAUMA.
 
Back
Top Bottom