Ally Bananga yupo Sahihi; Familia ndio jambo la kwanza

Ally Bananga yupo Sahihi; Familia ndio jambo la kwanza

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
ALLY BANANGA YUPO SAHIHI; FAMILIA KWANZA.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Kwa watu wasiojua maana ya familia, wasiojua maana ya ndoa ni rahisi kumponda na kumkosoa vikali Ally Bananga. Lakini kwa wanaojua maana ya familia, wanaojua maana ya Mke/mume na watoto ambao ndio familia yenyewe watamuunga mkono Bananga.

Kila tukifanyacho ni kwa ajili ya Wake/ Waume zetu pamoja na watoto wetu. Tunahangaika kwa ajili ya familia zetu, usiku kucha, mchana kutwa tunakimbizana na maisha kuhakikisha familia zetu zinafurahia uwepo wetu sisi kama Baba/Mama. Tunahakikisha Wake/waume zetu wanaona jinsi tunavyowapenda kwa vitendo na wala sio mdomo ambao hata kasuku anao.

Ally Bananga ameonyesha nguvu ya familia katika maisha. Huwezi penda nchi kama huipendi familia yako, huuo ni uongo. Huwezi kuwa mzalendo kama hupendi familia yako. Jamii zote zilizoendelea Dunia zinaelewa jambo hili. Huwezi pata baraka kwa kuipenda nchi ila unaweza pata baraka kwa kuipenda na kuijali familia yako. Baraka za familia yako ndizo zinainua taifa.

Mtu yeyote mwenye akili timamu awe mke/mume ukitaka kukosana naye basi iguse familia yake hapo ndio utaelewa nguvu ya familia.
Familia bora huunda taifa bora.

Wanaume wanaopenda familia zao huunda wanaume wanaopenda nchi yao.
Wanawake wanaopenda familia zao huunda wanawake wanaopenda nchi yao.

Huwezi penda nchi kama hupendi familia yako. Mwanaume yeyote asiyependa familia yake, anayeitesa kwa namna moja ama nyingi hasa kwa dhahiri kabisa, huwa mwanaume mbinafsi, na sio ajabu hata akipewa uongozi katika taifa akaleta ubinafsi wake na kudhuru maslahi ya nchi.
Mtu kama hapendi watoto wake na mke wake unafikiri ataipenda nchi yake?
Mtu kama hayupo upande wa watoto wake au mke/mume wake unafikiri atakuwa upande wa taifa lake?

Ally Bananga Yupo sahihi, na nafikiri viongozi wote wakubwa, na watu wenye upeo mkubwa wanamuelewa anazungumzia jambo gani. Labda walete siasa wanaweza jifanya hawamuelewi.

Mifano ya Watu waliosimama na Familia zao

1. Familia ya Adamu akiwa na mkewe Hawa

Katika Historia ya kidini tunaiona Familia ya Adamu ambayo inasadikika kuwa ndio familia ya kwanza kwa wafuasi wa dini za Abrahamu.
Baada ya Hawa kudanganywa na Nyota na kuingia dhambini. Tunaona akienda kwa mumewe Adamu.
Adamu naye anakula lile tunda sio kwa sababu amedanganywa au hajui matokeo, hasha! anajua, na wala hajadanganywa bali UPENDO ndio unamfanya aisikilize sauti ya Mke wake, Hawa na kisha kuidharau na kuiasi sauti ya MUNGU wake.
Adamu aliamua kufa pamoja na Mkewe Hawa kwa sababu alikuwa akimpenda sana. Hiyo ndio maana ya True love.

Licha ya Mungu kutoa adhabu zake lakini alijua alichokionyesha Adamu kwa mkewe ni UPENDO, na hii ilimaanisha kuwa ADAMU alikuwa akimpenda HAWA mkewe kuliko anavyompenda Mungu.
Amri hiyo hiyo Mungu anawaaigiza wanaume wote wawapende wake zao, hata hivyo haimaanishi kuwa wawapende zaidi kuliko kumpenda yeye, Mungu.

2. FAMILIA YA ABRAHAM NA MKEWE SARAH

Moja ya familia bora za kuigwa ni pamoja na Familia ya Ibrahimu. Licha ya changamoto za hapa na pale, madhaifu ya Sarah ya utasa wa muda mrefu lakini Bado tunaona Abraham alikuwa upande wa mkewe mwanzo mwisho. Hata Saraha alipompa ruhusa mumewe azae na Hajri bado Abraham alikuwa upande wa mkewe. Hata Sarah alipomuambia Ibrahimu amfukuze Hajri baada ya yeye kumpata Isaka, Ibrahimu alikubali kishingo upande lakini akashinikizwa na MUNGU kuwa awe upande wa Mkewe, yaani amsikilize mkewe SARAH.

Pia Sarah alikuwa upande wa mumewe kipindi wanaenda Misri, aliokoa maisha ya mumewe, Ibrahimu kwa kujifanya yeye ni Dada yake tuu.

3. FAMILIA YA EDWARD LOWASA NA MKEWE REGINA
Baada ya Lowasa kukatwa kichwa kwenye Chama chake cha CCM, Lowasa aliamua kuhamia CHADEMA, kitendo cha Mkewe Ragina kumuunga Mkono ilionyesha dhahiri kuwa familia ndio jambo namba moja kisha mengine ndio yafuate.
Hii ni tofauti na baadhi ya familia zile ambazo hazina umoja ambapo Baba anaweza kufanya maamuzi ya fulani na mpinzani mkubwa akawa mkewe na watoto, halikadhalika na mke kupingwa vikali na mume na watoto.

4. FAMILIA YA TUNDU LISU NA MKEWE ALICIA
Unajua kila mtu anaubora wake na udhaifu wake. Unapoamua kuolewa au kuoa sharti ukubali ubora na udhaifu wa mwenza wako. Unapoingia kwenye ndoa ni kwamba unautangazia ulimwengu na mbingu kuwa umeridhishwa na yote ya mwenza wako.
Ndio maana wakati mwingine kuachana haichukuliwi kama jambo zuri kwa sababu linaashiria kuwa hukufanya uchunguzi wa kutosha na ULIKURUPUKA.

Tundu lisu ni moja ya watu ambao nimekuwa nikiwasifia tangu nilipomfahamu. Tundu Lisu ubora wake na pengine ukawa udhaifu wake ni msimamo mkali ulipitiliza.

Kitendo cha Tundu lisu kuiandama serikali ya Hayatti Magufuli non- stop huku hatari ya kuangamizwa ikizidi kumkabili lakini Mkewe kukaa kimya siku zote kumaanisha alikuwa akikubaliana na Mumewe. Hata Alipogipwa Risasi bado tunamuona Bi. Alicia akiwa Bega kwa Bega na Mumewe mpaka kupona na kuja kugombea tena Urais, ni funzo kubwa sana.

Hii ni mifano michache kati ya mingi

Mkeo/Mumeo lazima uwe kitu kimoja naye haijalishi ni jambo zuri au jambo baya. Lazima uwe upande wake hasa ukiwa mbele za watu lakini mkiwa ndani ya nyumba ndio mnajadiliana na kurekebishana. Hiyo ndio maana ya Familia.

Bananga hajakosea labda kwa watu WANAFIKI.
Ingawaje hoja ninayoungana nayo kwa baadhi ya watu ni ile isemayo kuwa; hakuwa na sababu ya kueleza mambo hayo mbele za watu kwani ni jambo linalofahamika na ambalo halipingiki kwa watu wote wenye akili.

Wito; Kuipenda familia yako ndio kuipenda nchi yako. Kwani tunafanya kazi kila siku kwa ajili ya familia zetu, familia zetu zikiendelea nchi nayo inaendelea, familia zetu zikipuyanga nchi nayo itapuyanga.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa morogoro
--
Pia soma > Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu
 
Inajulikana wazi mkuu , unaanza kupenda familia , inakuja ukoo, kabila , Taifa alafu bara ........ Huwez kuruka stage , mfalme Daudi alikuwa under high criticism ya ukabila , imagine highest army commanders wote walikuwa watoto wa ndugu zake .....hata hvyo kipindi cha mjukuu wake issue iliishia Kwa makabila mengine kujitenga na kuanzisha nchi Yao ...... !! Hata Mimi nikiwa kiongozi lazima niwapendelee wa kwetu Kwanza siwez kumwacha kwenye njaa kisa et Taifa , huo usenge siwezi
 
Inajulikana wazi mkuu , unaanza kupenda familia , inakuja ukoo, kabila , Taifa alafu bara ........ Huwez kuruka stage , mfalme Daudi alikuwa under high criticism ya ukabila , imagine highest army commanders wote walikuwa watoto wa ndugu zake .....hata hvyo kipindi cha mjukuu wake issue iliishia Kwa makabila mengine kujitenga na kuanzisha nchi Yao ...... !! Hata Mimi nikiwa kiongozi lazima niwapendelee wa kwetu Kwanza siwez kumwacha kwenye njaa kisa et Taifa , huo usenge siwezi

😃😃😃😃😃

Hitimisho lako la kibabe mkuu
 
Back
Top Bottom