Pre GE2025 Ally Hapi akemea tabia watu kuuwana, kutekwa na kupotea katika mazingira yanayoibua sintofahamu

Pre GE2025 Ally Hapi akemea tabia watu kuuwana, kutekwa na kupotea katika mazingira yanayoibua sintofahamu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi, Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Hapi amekemea tabia inayoindelea kwa sasa ya watu kuuwana, kutekwa na kupotea katika mazingira yanayoibua sintofahamu na kuibua maswali mengi yasiyo na majibu katika jamii.

Hapi ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe ikiwa ni katika mwendelezo wa ziara yake mkoani humo inayolenga kuijenga Jumuiya ya Wazazi na Chama Chama Mapinduzi.

Soma Pia: Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu

..jamaa unaona kabisa kuwa ameishiwa hoja na sera.
 
Machoni kama watu! Kuna mwingine nasikia ametangaza kutoa sadaka huko kaskazini baada ya kukoswakoswa na wenzake!
 
Baada ya bunge na mahakama kukata na kutoonesha msaada wowote kuhusu watu kutekwa
Naona wananchi sahv wataamua kujilinda.....

Ova
 
Baada ya bunge na mahakama kukata na kutoonesha msaada wowote kuhusu watu kutekwa
Naona wananchi sahv wataamua kujilinda.....

Ova
Wananchi wamechelewa sana kulijua hili, imani kwa polisi imepungua sana na vyombo vingine. Kila mtu awe mlinzi
 
Wananchi wamechelewa sana kulijua hili, imani kwa polisi imepungua sana na vyombo vingine. Kila mtu awe mlinzi
Maana hizo mamlaka hazina msaada wanawaona wananchi
Kama mabwege tu

Ova
 
UK ni kanchi kadogo sana by AREA, Lakini hali ndiyo hii :-

The missing persons crisis is a silent epidemic across the UK. Around 170,000 people are reported missing every year – a figure that charities and police have long acknowledged as a significant underestimate. One disappearance is officially recorded every 90 seconds.
kila sekunde 90 nchini UK, anaripotiwa mtu ame dis appear!
 
Kuna mwamba mmoja hapo Kenya anaitwa Jimmy Wanjigi , katafutwa na police siku mbili nyumbani kwake bila mafanikio, walipoondoka akatoka na kuwahabarisha kuwa kamwe hawatoweza kumpata ndani ya jumba lake hilo la kifahari badala yake wakimhitaji wafuate taratibu za kisheria atatii bila shuruti.

Anampasua pasua Ruto kwa kumkosoa vilivyo kwenye media kuhusu kusua sua kwa uchumi wa Kenya
 
Yatupasa kumuomba Mungu wa Mbinguni atuhurumie

Naangalia hapa Citizen TV ni vilio vitupu vya Watu kuwatafuta Wapendwa wao bila mafanikio

Duh mlale usingizi wa mang'amu g'amu 🐼
Oya tupoteeni tu kama vip
 
Back
Top Bottom