PostGE2025 Ally Hapi: CHADEMA kila siku Katiba Mpya, Katiba Mpya inatuletea Ugali mezani? Wananchi wanataka hoja, siyo malalamiko

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Ally Salum Hapi akiwa Shinyanga Juni 4, 2026 amesema; "Chama chenye sera nzuri, ni chama cha Mapinduzi.

Wamepewa fursa ya kusema, waitumie fursa hiyo kusema. Lakini sasa saa nyingine mnashangaa, kila wakizungumza hawasemi shida za wakulima, hawazungumzii pembejeo.

Shinyanga hapa ni wakulima wa pamba, huwasikii wakizungumzia pamba. Wao kila siku tuahirishe uchaguzi, wao kila siku katiba mpya.

Sawa, lakini katiba mpya inatuletea ugali mezani? Lakini hiyo tume huru inaleta pembejeo kwa wakulima wa pamba?"

Your browser is not able to display this video.
 
Kwani ninyi mmeleta ugali mezani? Mawazo finyu kweli......Katiba ni sheria inayotuongoza. Kungekuwa na katiba mpya, msingeshinda kwa uongo na kura feki, msingeweza kuiba uchaguzi, ninyi ni wachezaji na refa pia....Muone aibu, wala hamkupaswa muongoze nchi hii wajinga ninyi hamna quality, wezi wa kura ninyi, na kila mtu anawajua. Kumbuka binadamu haishi kwa mkate tu, NINYI MNAWAZA UGALI TU. Kimsingi hamkutakiwa kushinda uchaguzi wowote ule.
 
Mwambieni afatilie mikutano yote mambo yote ya hovyo waliyotusababiahia yanazungumzwa yakiwemo mirahaba ya ajabu kwenye madini kifupi ccm hii ni genge la wapigaji tunapswa kuwafulusha mapema iwezekanavyo tutavuna mabua
 
Rudia maneno yako mara kumi kama wewe sii Yuda kwa Watanzania?
 
Yaaani huyu anaona kuleta ugali mezani ndio key issue? Katiba mpya is about the future

Kama anataka ugali akalime mahindi
 
Katiba mpya ni ya wananchi Sio CHADEMA!
 
Kikubwa amekiri kuwa hakuna TUME HURU YA UCHAGUZI.
Sasa bila tume huru ya uchaguzi wataingiaje madarakani kuongoza nchi ili wafanye hayo mambo mbadala?
 
Je hizo sera zenu nzuri zimeleta ugali mezani? Sera zenu nzuri ndiyo Bunge la ulaya limewanyima misaada? Sera zenu nzuri ndiyo zimeua maelfu ya vijana/wazazi/watoto Mo29?
 
Ally Hapi ana kandamiza right left and center vizuri sana aise dah!🀣

well done hapi πŸ‘Š
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ CCM ni vilaza, kwani lazima kila mtu azungumzie kilimo.
 
Imagine akili hizi eti ndio za kuwaongoza watanzania 🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…