Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Salum Hapi, amesema kauli ya Mary Chatanda kuhusu kuwafuta CHADEMA ilikuwa ni tambo za kisiasa na haipaswi kutafsiriwa kama yenye nia mbaya. Hapi amesema hakufahamu muktadha kamili wa kauli hiyo kwa kuwa hakuiona video ya Chatanda akieleza, hivyo hawezi kutoa msimamo wa kina kuhusu alichokusudia.
“Nadhani ni tambo za kisiasa tu,” amesema Hapi, akibainisha kuwa kauli hiyo inaweza kuwa sehemu ya ushindani wa kisiasa kuelekea uchaguzi ujao. Amesema anaamini kauli hiyo ilikuwa na lengo la kuonyesha dhamira ya kisiasa ya CCM kushinda majimbo mengi, ikiwemo ya mijini, badala ya kuwa na maana nyingine yoyote yenye nia mbaya.
Soma: Mary Chatanda: Samia angenipa nchi dakika moja, ningeimaliza CHADEMA