PreGE2025 Ally Hapi: Rais Samia amefanya kazi kubwa katika Afya, amejenga Hospitali za Wilaya 129, Vituo vya Afya 485

PreGE2025 Ally Hapi: Rais Samia amefanya kazi kubwa katika Afya, amejenga Hospitali za Wilaya 129, Vituo vya Afya 485

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Ally Hapi, amesema Rais wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan anastahili pongezi kwa juhudi zake katika kuboresha sekta ya afya nchini ndani ya miaka minne ya uongozi wake.

Akizungumza katika Kongamano la kumpongeza Rais Samia kwa kutimiza miaka minne madarakani lililofanyika siku ya Jumanne mkoani Arusha, Hapi amesema kuwa jitihada za Rais Samia zimekuwa kielelezo cha kupambana na moja ya maadui wakuu wa taifa ikiwamo maradhi.

"Baba wa Taifa aliwahi kusema kwamba tunao maadui wakubwa watatu: ujinga, umasikini na maradhi. Inawezekana tunao maadui wengi lakini hao ni wakubwa zaidi. Rais Samia amefanya kazi kubwa kupambana na adui maradhi kwa kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi, huku vituo vya afya vikiboreshwa ili kutoa huduma za kisasa," amesema Hapi.

Ameeleza kuwa ndani ya kipindi cha miaka minne, Rais Samia amefanikisha ujenzi wa hospitali za wilaya 129 na vituo vya afya 485 katika kata mbalimbali nchini.

"Katika kipindi chake, kila Halmashauri nchini imepata magari mawili mapya ya kisasa kwa ajili ya huduma za afya. Jirani zetu Wakenya walikuja kujifunza jinsi Rais Samia alivyoleta mageuzi katika sekta ya afya," ameongeza Hapi.
 
Ambacho nakiona mimi kwa wanasisiem mimi naamini kabisa wapo kwa ajili ya njaa binafi na sio njaa za wananchi.
Na kwa upeo na mapambio yanayotolewa kila siku as if mama na malaika hana doa lolote la hasha ni binadamu kama walivyo binadamu wengine. Hivyo basi kuna maamuzi lazima akosee kama mwanadamu,
Kuwa rais hakumuondelei ubinadamu wake. Kuwa rais hakumfanyi yeye asikosee. Pamoja na hayo yote, sisiem hawana ubavu wa kumkosoa rais hata kama amekosea, kinachobaki ni mapambio masaa 24, wenzenu tumechoka na hayo mapambio. Tunajua why mapambio, tumbo njaa.
 
Hata ajenge Daraja la Dhahabu kutoka Dar hadi Kizimkazi sisi tunachotaka ashinde kihalali sio kuwatuma akina Mchengerwa waharibu chaguzi.
 
Hata Magu, alimsifia sana, mpaka akafikia kutishia kuwapiga wastaafu, kwa waliokuwa wanamkosoa!
 
Back
Top Bottom