Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Hapi amesema katika utekelezaji wa Bima ya Afya kwa wote, changamoto zote zilizopo sasa kuhusiana na bima ikiwemo baadhi ya Maradhi kutotibiwa kwa Bima zitatatuliwa na bima hiyo itaweza kulipiamatibabu kwa magonjwa yote makubwa ikiwemo figo, moyo na saratani
Akizungumza leo Septemba 27, 2025 kwenye kipindi cha Cafetalk Jijini Dar es salaam kilichokuwa kikijadili, Je? Serikali ya awamu ya Sita imeweza kugusa maisha ya Watanzania? Hapi amesema ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa kwa Rais (Dkt. Samia Suluhu Hassan akishinda) serikali itakuwa imekamilisha mchakato wa bima hiyo
"Mapungufu ya bima kwa hali ya sasa na Vifurushi vyake, nadhani tumekwisha kueleza ndani ya siku 100, Kansa, Magonjwa ya Moyo, Figo na Sukari, magonjwa yote makubwa ambayo yamekuwa ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania, haya yote gharama zote za Matibabu zinakwenda kubebwa na Serikali" amesema Hapi
Soma pia GE2025 - Ally Hapi: Siku 100 za Rais Samia Zitamaliza Changamoto za Bima ya Afya