Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amesema "Tusidanganyike tukaharibu nchi yetu yakatukuka kama ya Libya kwa Gaddafi". Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja me wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano wa hadhara, ambapo amewasihi Watanzania kulinda amani na utulivu uliopo nchini.
Katika hotuba yake, Hapi alieleza mfano wa nchi ya Libya kabla na baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kiongozi wake Muammar Gaddafi, akibainisha kuwa Libya ilikuwa nchi yenye uchumi imara na maisha mazuri kwa wananchi wake, ikiwemo huduma za afya, elimu na maji bure.
Soma > Ally Hapi: Rais endelea na kazi, CHADEMA tuachie sisi
Hata hivyo, kutokana na ushawishi wa nje na msukumo wa mabadiliko bila kutafakari madhara yake, nchi hiyo ilitumbukia kwenye machafuko na vita ambavyo hadi leo vimeharibu amani na uchumi wao.