Ally Kamwe chukua tahadhari, Manara kuhamasisha gemu ya Yanga vs TP Mazembe ni udhaifu wako kiutendaji, usiruhusu hilo

Ally Kamwe chukua tahadhari, Manara kuhamasisha gemu ya Yanga vs TP Mazembe ni udhaifu wako kiutendaji, usiruhusu hilo

Wewe ndio afisa habari wa Yanga, wewe ndio unatakiwa upite kwenye media zote ushawishi wanaYanga waende disband kuishangilia Yanga mwanzo mwisho, kazi hiyo unaiweza vizuri sana.

Wewe umeaminiwa na taasisi kubwa ya michezo nchini, Yanga, wananchi wanakukubali sana wewe.

Wakati wanaYanga wanajiuliza nani semaji baina yako na Manara wananchi walikuwa pamoja na wewe mwanzo mwisho.

Gusa achia twende kwao ni wewe ndio umeifanya kazi hiyo hadi bendi za muziki nazo zinaimba.

Sasa hivi wewe una followers wengi kutokana na wananchi kukuelewa sana ndugu yangu.

Lakini hili la kumruhusu Manara akusemee kwenye media zote ahamasishe watu kwenda uwanjani huku kesho akienda Wasafi kuhamasisha, u napoteza mvuto kaka.

Kipi kimekufanya ushindwe kwenda kwenye media kuhamasisha na umemuachia zungu pori?

Wengi watashindwa kwenda uwanjani kwa sababu huyo zungu pori akihamasisha na watu wakijaa uwanjani badala ya kupongeza mashabiki na wenzake kwa kazi kubwa walioifanya, anaanza kujisifia yeye kuwa ndio amejaza watu uwanjani.

Jiandae kaka huo ni mwanzo, anytime huyo mwarabu wa nguruka atachukua nafasi hiyo.
Ukubali ukatae Manara pekee, narudia manara pekee ndiye mhamasishaji bora wa wakati wote.

Manara ameongeza sana hamasa ya mpira nchini.
Uache unafiki kijana
 
Lengo ni kuhamasisha watu waende uwanjani, awe kamwe, manara au mtu yoyote ikibidi waongezeke watu waende kwenye media zingine kufanya hamasa nyingi iwezekanavyo, watu wakijaa mapato yataongezeka club itapata faida.Hizo personal issues si muhimu.
 
Wote waongee tu maana hawana chochote kinachoweza kuidhuru timu yetu, tunategemea sana benchi la ufundi.
 
Haji mzee wa fitna anazeeka vibaya
 

Attachments

  • FB_IMG_1713799997765.jpg
    FB_IMG_1713799997765.jpg
    53.3 KB · Views: 4
Dunaini kote shabiki anaenda uwanjani kwa mapenzi yake kwa timu
acheni uswahili, Taifa limejaa waswahili sana sijui lini watapungua.

Kuhamaisha eti shabiki aende uwanjani ni ujinga.
Kwahiyo Yanga haina wapenzi wa kwenda uwanjani? Maana hata Yanga iwe inafanya vizuri kwenye performance bado unaona kabisa uwanja haujai. Usilinganishe na nchi za wenzetu huko, soka la Tanzania limejaa hamasa ya ushawishi ukiacha na matokeo ya uwanjani.
 
Back
Top Bottom