Ally Kamwe haaminiki, aliwadanganya Utopolo kuhusu beki la CHAN na sasa wanamuamini tena kuhusu Namba 06

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Sisi waislam tumefundishwa kuwa alama za mtu mnafiki ni tatu, kwanza akisema hatekelezi, Pili ahadi zake za uongo.

Ally Kamwe ameingiza tena mjini wanachama na mashabiki wa Utopolo kuwa timu yake inaleta kiungo namba 6 ambaye hajawahi kutokea!

Hi kuna namba 6 pale Yanga aliewahi kumzidi Marehem Method Mogella Fundi? Kuna namba 6 Yanga aliewahi kumshinda marehemu Issa Athuman? Kulikuwa na Geofrey Bonny, huyo anayemtaja yeye ni kutafuta Kiki tu.

Kumbukeni watu wa Utopolo walihamanika kishenzi alipowaambia kuwa kuna beki la CHAN limekuja Jangwani, watu wakaamini lkn mwishowe beki la CHAN likaishia kukaa benchi msimu wote huku sana sana likipangwa kwenye mechi za kirafiki na zile za kumalizia msimu ambapo Utopolo walishatawazwa mabingwa.

Beki la CHAN Mamodou Doumbia likaishia kubeba mifuko ya simenti kama kawaida yao Utopolo wakidai wanatoa kwa jamii.

Leo wanadanganya kwenye mkutano mkuu wa kujadili masuala nyeti ya klabu na kuwatoa mchezoni wale wanachama werevu kuwa kuna mido namba 6 anaingia nchini na hajawahi kutokea, eti it is unprecedented.Pumbavu kabisa.
 
Hofu ya mido namba 6 imekwisha wajaa mapafuni.

Mmoja mmoja wanaanza kujitokeza.

Wakifikiria bajeti ya Bil 20 wanakosa raha kabisa.
 
Sasa si bora hiyo ya Beki wa Chan tunaweza kusema ni utani wa hapa na pale kwasababu amesema Afisa habari ambaye kazi yake ni kulopoka.

Vipi kuhusu ule uzinduzi wa Yanga Tv kwenye king'amuzi cha Azam ulioongozwa na Raisi wa Club?

Au wenzangu huko kwenye ving'amuzi vyenu hiyo channel ipo?
 
Yaani kaka povu lote hili?

Kwann usimuwekee hili povu mudi aliyewalostisha misimu 2 iliyopita

Kaka No matter what, Yanga wamewaweza na mkicheza watazidi kuwaweza. Jengeni timu acha kufatilia mambo ya Yanga. Acha wanachama wa Yanga wamuhukumu Ally, usijipe hiyo kazi. Hawajakuomba na huna sababu kuwasemea, JISEMEE MAMBO YENU!
 
Mimi nilichoelewa ni kwamba mchezaji atavaa jezi No.6. Ila sijasikia ikisemwa atacheza No.6. Hao wote uliowataja walicheza No.6 na wengine kama ISSA alivaa No.4 mgongoni.
 
Waliahidi kocha la makombe, mwisho wa siku tumeletewa kocha ambaye hata Matola anamzidi kwa makombe.
 
Wametuweza wapi huku tumewafunga nje ndani kwenye ligi kuu
 
Ipo chanel ya bilioni 20 tuliyodanganywa na mhindi kuwa ipo benk lakini aijulikani ni benk gani, ni bora waliodanganywa na chanel lakini makombe yanajaa kabatini vipi wale wa bilioni 20?
 
Sasa unaumia nini kaja haja perform ila makombe tumebeba.

Wewe cha msingi msubirie jamaa atakavyo uwasha, endelea kuwa mvumilivu.
 
Umenikumbusha kaka yangu Godfrey Bony Mwandaje ticha 2007-2010.

Huyo kamwe yeye ni KUROPOKA ROPOKA.

Amekuwa WA HOVYO mno
 
Huko kweli wenye akili ni wawili tu, kwani nyie hamumseni sawadogo? Mnasahau mlisajili mtu kutoka nyu kesto
 
Ukituambia Bil 20 za Mwamedi ziko benki gani utaambiwa kuhusu uzinduzi wa Yanga tv.
 
Ipo chanel ya bilioni 20 tuliyodanganywa na mhindi kuwa ipo benk lakini aijulikani ni benk gani, ni bora waliodanganywa na chanel lakini makombe yanajaa kabatini vipi wale wa bilioni 20?
Umepuyanga topolo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…