Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga SC Ally Kamwe amewataka Mashabiki wa klabu hiyo kusimama na kuinua mkono mmoja juu ikifika dakika ya [emoji2393] kuonyesha ishara ya vidole vitano katika mchezo wa kesho dhidi ya Coastal ikiwa ni ishara ya kuwapongeza Wachezaji wa klabu hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwenye ushindi wa 5-1 dhidi ya Watani wao Simba SC.
“Mashabiki wa @YoungAfricansSC tutakaoingia Mkwakwani kesho, Tunaombwa ikifika DAKIKA YA 5 kwenye mchezo wetu Vs Coastal Union Tusimame wote na kuinua mkono mmoja juu tukionyesha ishara ya vidole vitano Hii ni kwa ajili ya kuwapongeza Wachezaji wetu kwa kazi nzuri waliyoifanya” ameandika Ally Kamwe kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.
[emoji3578] Una maoni gani kuhusu hatua hiyo ya Kamwe?
#KitengeSports
View attachment 2807614