Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break. Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break. Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
BAADA YA KUDHIHAKIWA NA ALIKAMWE, JUMA MGUNDA AMPA JIBU

🗣️"Yanga ni Club yetu pekee Tanzania inayotuwakilisha kwenye fainaly hii ya CAF na kwa bahati iliyonjema inacheza na Club Inayotoka nje ya nchi yetu.

🗣️Sijui kinachopelekea mimi kuwa miongoni mwa kampeni hii ya matusi na kunidhalilisha Nilidhani kampeni itakuwa ni kushinda fainally , kuliko hiki alichokifanya Mwanangu Ally Kamwe.

🗣️Namuombea kwa Mungu awe na mwisho mzuri , mimi nimeshuhudia watu wengi wakifanya kazi Yanga na Simba na sasa wapo nje ya mfumo.

🗣️Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie .

🗣️Tusiposhinda kesho nitashangaa sana kwanini tumefungwa wakati kilichotakiwa kifanywe kimefanywa juu yangu na familia yangu" Kocha Juma Mgunda.

Akiwa ktk kampeni za mechi ya tarehe 28/05/2023 huko Zakhiem Mbagala aliwauliza mashaabiki kati ya "Mgunda na andazi" utachagua nini. Mashaabiki wakaitikia "andazi" . Hakutosheka akauliza tena"kati ya wasimamizi wa Feisal na andazi nini. Mashaabiki tena wakajibu "andazi".

Sasa mimi km mtu mzima naona Ally Kamwe alichofanya ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa malezi na makuzi ya wazazi wake. Huwezi kumlinganisha mtu mzima mwenye umri sawa na baba yako na "andazi". Mgunda amekuwa Hana utani wa Simba na Yanga hata ktk media sjawahi kumskia akitoa maneno ya shobo kwa Wana Yanga. Iweje leo mbele ya watu tena wa rika tofauti tofauti umlinganishe na andazi.

Haya sasa kakujibu kiutu uzima km baba. Kazi kwako.
 
Simba na Yanga kutaniana tania ni jadi,wala sio serious issue ni kutaniana tu,haimaaniishi chochote,
 
Wenye shida ni hao mashabiki waliochagua ANDAZI. Ali yeye aliuza tu.
Kama mashabiki wangechagua tofauti kungekuwa na povu kama hili kwa Ali?
Na hata hivyo hawalaumiki, kila mtu anachagua akipendacho, hakuna kupangiana.
 
Inabidi utani uwe kwenye simba au yanga yenyewe na usiwe kwa mtu binafsi
Mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu.
Yule msemaji wa Nganda aliesema wenye akili Yanga ni baba yake tu baadae akajirudi kidogo akamjumuisha na Kikwete, waliobaki wote hamnazo, pale imetaniwa timu au wametukanwa watu?
Hivi vitu si vyakuchukulia serious saaana.
 
Ukishakaa na Manara tu ni lazima urukwe akili.

Mpaka sasa wasemaji bora ni Masao Bwire na Mzee Kifaru wa Mtibwa.

Si Ahmed Ally wala huyo Ally Kamwe wote ni takataka tu.

Simba kama wako serious wamchukuwe Masao Bwire ndio anafit kwenye brand ya Simba.

Mtakaomsakama Ally Kamwe msijizime rada Simba ndio wana kimeo zaidi huyo Ahmed Ally kuliko hata Ally Kamwe.

Haya yote ni madhara ya muda mrefu sana yatatuandama kwa kumuacha mpuuzi kama Manara atengeneze chuki kwenye mpira wa Tanzania.
 
Kuna watu wanatafuta faraja kwa namna yoyote ile baada ya kutoka sifuri msimu huu! Mara michango mara Mgunda! Ishu ndogo wataikuza ilimradi wafarijike tu!
 
Mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu.
Yule msemaji wa Nganda aliesema wenye akili Yanga ni baba yake tu baadae akajirudi kidogo akamjumuisha na Kikwete, waliobaki wote hamnazo, pale imetaniwa timu au wametukanwa watu?
Hivi vitu si vyakuchukulia serious saaana.

Hauoni kama hakutaja jina la mtu tofauti na kenge maji huyo
 
Sasa simlimchukua maana mlikubaliana na maneno yake.

Kama angekuwa kasema uongo sidhani kama mngekuwa nae huko kilingeni kwenu.
 
Sasa simlimchukua maana mlikubaliana na maneno yake.

Kama angekuwa kasema uongo sidhani kama mngekuwa nae huko kilingeni kwenu.
Alichukuliwa na GSM sio Yanga.
Na tajiri hanuniwi, tumeyaona haya hata kwa Madunduka na mlio wao wa ng'ombe.
 
Hauoni kama hakutaja jina la mtu tofauti na kenge maji huyo
Angesema baadhi ya washabiki wa Yanga ni..., hapo ingekuwa hakutaja jina, kwasababu hao baadhi itakuwa hawajulikani nani na nani hasa.
Lakini unataja majina ya watu 2 unasema hawa hawamo, waliobaki woooote wamo, hapo vipi utasema hakutaja jina wakati wasiokua hao wawili wanafahamika?
 
Back
Top Bottom