Utopolo na Makolokolo ni legasi ya Manara,
Hadi kesho, sisi washabiki tunaitumia hiyo misemo! Na imekuwa nembo za utani wa Simba na Yanga
Pia usisahau msemo wa " Yanga wenye akili ni Kikwete na Sunday Manara!"
Msemo ambao ni nembo ya mashabiki wa Simba
Falsafa ya Manara ktk uafisa habari Ilikuwa Ni Habari na utani wa KUKERAA
Na sisi washabiki tulikuwa tunasema "Manara Wakereee!
Alipokuwa Simba aliwakera Sana yanga
Alipokuwa Yanga aliwakera Sana Simba
Maadam amewakera pande zote, Simba na yanga
Na maadam watanzania wote ni Simba na Yanga,
Manara ametengeneza vidonda pande zote na amejikuta amechukiwa na wengi, ukiwemo wewe mleta mada
Manara ana legasi kubwa ktk tasnia ya usemaji wa Club
Hao wasemaji wa Sasa unao wasifia wafuatilie vizuri, utagundua nao wanafuata falsafa ileile ya Manara ya Uafisa habari wa kukera!
Wafuatilie vizuri utagundua!
Hata hii nyuzi yako inaonesha jinsi Manara alivyoteka anga la habari za Michezo Tanzania
Ila nikukumbushe, kila lenye mwanzo Lina mwisho!
Labda Sasa, jua la Manara linazama! Ni kawaida kwenye maisha,
Walipita wasemaji wengi Simba na Yanga na waliondoka, na Sasa si ajabu Manara kuondoka!
Usimtazame Manara kanakwamba alikuwa na haki ya kudumu kwenye kitengo Cha usemaji milele
Hao wasemaji wa Sasa nao wataondoka
Hata wewe mshabiki utaondoka na watakuja washabiki wengine!