Ally Kamwe: Shabiki anayeweza kuwa mshambuliaji aje atusaidie mechi dhidi ya Mtibwa Sugar

Ally Kamwe: Shabiki anayeweza kuwa mshambuliaji aje atusaidie mechi dhidi ya Mtibwa Sugar

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Kikosi cha Klabu ya Yanga kimewasili jijini Dodoma kwa ajili ya kuwakabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara utakaochezwa March 21 kwenye Uwanja wa CCM Jamhuri, jijini Dodoma

Akizungumza mara baada ya kuwasili, Afisa Habari wa klabu hiyo, Ally Kamwe, amesema dhamira yao ni kupata ushindi licha ya kuamini kuwa mchezo utakuwa mgumu kutokana na Mtibwa Sugar kuwa na muda mzuri wa kujiandaa.

Aidha, Kamwe amebainisha kukosekana kwa baadhi ya nyota katika kikosi hicho, akiwemo Prince Dube pamoja na Depu, hali inayowalazimu kuingia katika mchezo huo bila mshambuliaji halisi.Ambapo Kamwe amewaomba wanachama na klabu hiyo kama yupo mshambuliaji ajitokoze kwenda kuongeza nguvu katika kikosi hicho dhidi ya Mtibwa Sugar.
 
Anawakosea washambuliaji waliopo kwani mwanengo si mshambuliaji,guba,okelo,pacome na viungo washambuliaji waliopo hawatoshi?
 
shida sio mshambuliaji kuna huyu wa 12 mchezaji n balaa omben sanaaaa
RUNGU LINGINE ..

- Mwamuzi wa kati Ally Mnyupe amefungiwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu kwenye mechi ya NBC PL 🇹🇿 kati ya Azam vs. Yanga

- Mnyupe alishindwa kutafsiri sheria baada ya Fuentes kumchezea rafu Dube kwenye eneo la penati.

Follow #wolfsportnews
 
Karudie tena kusoma mada labda utaambua kitu.
Ko wewe alichokisema Ali kamwe umemuelewa vizuri?msemaji badala awatie moyo na hamasa zaidi washambuliaji waliopo na ili watoe uwezo wao wote kutikiza majukumu Yao bado anawaona hawatoshi kwani walisajiliwa kuja kufanyeje.Huu ndo muda wa wachezaji wengine ambao walikua hawapati namba kumuonesha mwalimu kwamba wanaweza.
 
Yeye amesema timu kwa sasa haina mshambuliaji asili yani namba 9, ila wewe umeelewa amesema timu haina washambuliaji!!.
 
Nipo hapa retired striker. Nipeni mkataba wa miaka miwili.
 
Back
Top Bottom