Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mbunge wa Zamani Wa Nkasi kaskazini Ally Keissy aliyekuwa na kila aina ya vituko na Mbwembwe ndani ya Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania,amesema ya kuwa anajipanga tena kugombea ubunge hapo Mwakani na kwamba hajaondoa dhamira hiyo.
Amesema mbunge aliyepo kwa sasa ameshindwa kutekeleza miradi mbalimbali ambayo yeye alikuwa ameibuni kwa ajili ya wana Nkasi.
Itakumbukwa ya Kuwa Mbunge huyo wa Zamani aliyehudumu kwa vipindi vitatu alidondoshwa chini na Mwana Mama kutoka CHADEMA Aida Khenani aliyepata kura elfu 21,229 ,huku Ally Keissy kutoka CCM akipata kura Elfu 19,972.
Mbunge huyo pia anakumbukwa kwa kauli zake na matukio yake mbalimbali ikiwepo yale ya kutifuana kikauli na wabunge wa kutokea Zanzibar mpaka kufikia hatua ya kunusurika kupigwa ngumi . Lakini pia amewahi kuwa gumzo na kuleta mijadala mitaani mikali sana juu ya kutaka na kupendekeza kubadilisha katiba ili kumuongezea muda wa kuongoza na kutawala Rais.kwa kauli kuwa katiba siyo msaafu au Biblia.
Nini Maoni yako juu ya Nia ya Mheshimiwa Mstaafu wa Ubunge kutaka kurejea tena Bungeni.Una mshauri agombee au awaachie wengine kutoka CCM waje na mawazo mapya na nguvu mpya ili yeye abakie tu kama mshauri. Ni kwanini mtu akiingia bungeni hataki kukubali kukaa pembeni ili kupisha wengine kama ilivyo kwenye Urais. Bungeni kuna nini ndugu zanguni ambacho wengine hawataki kuwapa hata nafasi vijana ili wakapeleke mawazo yao huko.
Nauliza tu ndugu zanguni kwa lengo zuri tu.Hii hapa ni picha yake wakati huo akiwa Bungeni
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.