Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani kinachowarudisha nyuma watanzania wengi hasa wenye vipaji ni baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya wenzao.ALI KIBA NA MADANSA WAKE WANUSURIKA KATIKA AJALI YA GARI!
![]()
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ali Kiba pamoja na madansa wake alfajiri ya jana(Jumapili) wamenusurika vifo kufuatia kupata ajali ya gari katika eneo la Mikumi mkoani Morogoro walipokuwa safarini kutokea Mbeya kuelekea jijini Dar-es-salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika gazeti la Nipashe ambazo BC imeweza kuzithibitisha kutoka kwa Ali Kiba mwenyewe,jumla ya watu saba wamejeruhiwa katika ajali hiyo huku watatu kati yao wamelazwa katika hospitali ya mkoa Morogoro.Ali Kiba ambaye aliumia mguuni na mkononi tayari ameruhusiwa kutoka hospitali na amesharejea nyumbani kwake Dar ambapo ameieleza BC kwamba anaendelea vyema. Ali Kiba alikuwa awe miongoni mwa wasanii waliotumbuiza katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyikia CCM Kirumba Mwanza hapo jana.
Chanzo kamili cha ajali hiyo hakijawekwa wazi na polisi tayari wanachunguza.BC inawatakia wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo kupona haraka ili waweze kurejea katika kazi zao.