Ukitaka kumpatanisha diamondi na Ali, waondoe watu walio mzunguka Ali kwani wengi wana chuki na diamondi
Ondoa tim Kiba, ondoa Ruge wa cloud(anakuza bifu kwa sababu zake binafsi) na queen wao Jokate (ni ex wa diamond hawakiachana vyema hawa), kama akiendelea kuwa na watu hao hawawezi kuja kupatana. Mashabiki wa kiba asilimia 99 ni wanao mchukia diamond, kuthibitsha hilo mbona Kiba alikuwepo kabla ya domo ila tim Kiba haikuwepo, yaan msanii atoke kisanaa mwaka 2006 halafu timu iundwe 2014!!! Na ukumbuke kipindi hiko Kiba alikuwa wamoto pia tena akipambana na Marlaw.
Kwa diamondi unahitaji kumtuliza tu Sallam huyu ndio huwa anakuwaga na kimuhe muhe na Kiba bila sababu, sasa huwa ana saidia kumkuza Kiba bila kujua atulie na yeye.
Kiba ni mkongwe ana miaka takriban 10 kwenye gem hana haja ya kutegemea bifu na msanii wa kimataifa Diamond ili kuweka jina lake juu tena akumbuke diamond kamkuta yeye kwenye gem. Diamond pia ni msanii wa kimataifa sasa kwa nini ana pick fights na local musicians!!!? Ajiamini naye sasa.
Hebu wapatanishwe sasa.