Ally Mayayi na kundi lako, uchaguzi ni mbinu na wala si makelele ya wapambe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nilikuwa nawaangalia kwa dharau sana kwa jinsi mlivyokuwa mnajibaraguza kwenye media , nilijua mtashindwa vibaya sana ! Kwanza ni bahati kupata hata kura 9 .

Mmeingia kwenye uchaguzi hata bila kuwajua wapiga kura , kampeni mngefanyaje ? Si umeona Karia wala hajahangaika na media zenu , alichofanya ni kuchukua kura za mtu aliyewekwa gerezani na kujipa yeye , baaasi !!!

Siku nyingine mje kuomba ushauri .
 
Nchi systems ndio zinatuua kuanzia sekta binafsi, serikalini mpaka TFF kama haupo ktk system hata uwe unajua vipi hupewi nafasi na ndicho kilichomkuta Ali mayay tembelea sio kwamba hajui tatizo hayupo ktk system (hizi system zimejaa vilazer kibao mmoja wao ni huyo karia) ,

Ila mwenzake karia systems imembeba na yy ana kazi ya kurudisha fadhila kwa walio mbeba, sasa usishangae Ruta akapewa tena mshauri wa maswala ya ufundi wa Rais, wakati hajawahi kucheza mpira hata wa mtaani wala kuhudhuria kozi yoyote (namjua nje ndani Ruta) huku wakiwaacha akina kibadeni wanaojua maswala ya ufundi. Subirini muone hizo kamati zitakazoundwa,

hazitozingatia uweledi bali ni za kulipana fadhila. Mpira wa Tanzania ujanja mwingi, jpili ndugu zangu simba wamepelekwa pelekwa na wakaambiwa hamna kuuliza maswala ya mapato na matumizi, huku ajenda kumi na nne zikijadiliwa ndani ya masaa manne si upuuzi huu.
 
Hahaaaaa...Umenena hapa..

Eti waliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kampeni ya 'Turudishieni Mpira wetu'..

Walitaka kutumia 'Ufaza' kuchaguliwa..Hawajui uchaguzi ni Ilani, Mipango na Mikakati..
 
Ndio maana nikawaambia next time waje wachukue ushauri .
 
Hahaaaaa...Umenena hapa..

Eti waliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kampeni ya 'Turudishieni Mpira wetu'..

Walitaka kutumia 'Ufaza' kuchaguliwa..Hawajui uchaguzi ni Ilani, Mipango na Mikakati..
Yes! Walikua wanafaa sana kuongoza but zile dambwi dambwi za uchaguzi n propaganda ziliwashinda
 
Kwa wajumbe walee, ambao Wallace Karia alifanya nao kazi na kuwajua vizuri, ulikuwa muujiza tu kwa yeyote kumshinda..
Wale wote walikuwa wampigie Malinzi , sasa baada ya Malinzi kuwekwa sero wakawa hawana mwenyewe , ndio maana wamempa Karia , tena kwa maelekezo ya Malinzi Mwenyewe kutokea sero .
 
Kwann usingewapa ushauri mwanzo?
Sikuwataka maana ukiacha kupiga danadana hawana ujuzi wowote na mambo ya uongozi .

Mshauri wao Julio ana kashfa ya kula hela ya Kajumulo .
 
Ruta tayari ameshafukuzwa kazi pale TFF, hakupiga kura na vyeti vyake vipo mikononi mwa vyombo vya uchunguzi
 
Ruta tayari ameshafukuzwa kazi pale TFF, hakupiga kura na vyeti vyake vipo mikononi mwa vyombo vya uchunguzi
Anaitwa Pelegrinus Rutahyuga...Eti alikuwa Mshauri wa Ufundi wa Rais wa TFF...Wizi mtupu
 
Anaitwa Pelegrinus Rutahyugak...Eti alikuwa Mshauri wa Ufundi wa Rais wa TFF...Wizi mtupu
Pyutuh, eti mshauri wa Rais mwenye elimu ya mashaka! Ama kweli soka letu lilikuwa shimoni. Linahitaji kazi ya ziada kulifufua.
 
TFF ni genge la wa wanyang'anyi..majizi sio rahisi mtu wa kweli kuingia
 
Hahaaaaa...Umenena hapa..

Eti waliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kampeni ya 'Turudishieni Mpira wetu'..

Walitaka kutumia 'Ufaza' kuchaguliwa..Hawajui uchaguzi ni Ilani, Mipango na Mikakati..
Bora wangesema "mpira ni haki yetu sote" kuliko "turudishieni mpira wetu" walienda chaka na slogan yao.Isitoshe wapiga kura na Karia ni mtu na boss wake na zimwi likujualo halikuli likakwisha,wao hawakuyajua hayo.Mpira ni wetu sote,hawakutakiwa kuja na slogan yya kutaka kuwatenga wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
True !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…