Ally Msengi amesajiliwa na klabu ya Stellenbosch ya Ligi Kuu Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu

kibol

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
4,521
Reaction score
2,747
KIUNGO mkabaji chipupizi wa Tanzania, Ally Msengi amesajiliwa na klabu ya Stellenbosch ya Ligi Kuu Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Kinondoni Municipal Council (KMC) ya Dar es Salaam.
Mratibu wa kampuni ya Siyavuma Sports Group, Michael Mwebe ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Msengi alizivutia klabu kadhaa za Afrika Kusini kabla ya kuamua kumwaga wino Stellenbosch baada ya kocha wa klabu hio kuonesha imani kubwa ya kumpa nafasi katika kikosi chake.
Msengi ambaye amezichezea timu zote za vijana za taifa kuanzia U17 na 20 anatarajiwa kuanza rasmi maisha mapya Katika Ligi Kuu Afrika Kusini Jumapili ya keshokutwa.
“Msengi anaanza ukurasa mpya baada ya kufanya vizuri akiwa na klabu ya KMC aliyoichezea kwa takriban msimu mmoja na nusu. Tunaushukuru uongozi wa KMC kwa ushirikiano mkubwa tangu alipotua hapo na pia kumpa baraka zote za kuondoka klabu kwa ajili ya kucheza soka nje ya mipaka ya Tanzania.
Siyavuma inaendelea kuamini katika vipaji vya vijana wa Tanzania, Msengi akiwa muendelezo wetu wa kuwapatia fursa ya kucheza soka la nje ya nchi. Ikumbukwe tulianza na Abdi Banda tuliyemtoa Simba na kumpeleka Baroka, baadaye Himid Mao, Eliud Ambokile, Yahya Zaydi na sasa Msengi” amesema Mwebe.
 
hivi Kagere kwa nini timu kubwa hazimtaki atastaafia hapo simba
Huu uzi ni mahususi kwa ajili ya Ally Msengi, kama una hoja kuhusu Kagere si vibaya ukaleta hiyo hoja kwenye uzi mwingine nami nitakuja huko kuchangia, tusubiri Januari 4 atakapowapa tena dozi ndio ataenda timu kubwa.
 
Hilo lizee nani alitake, hebu wacha utani wewe, huyo anamalizia mpira wake hapo hapo.
Ujinga wa viongozi wa Yanga Afrika ndio umesababisha ngasa analia njaa leo, mlimdanganya asisaini El merekh leo mnawapa kipaumbele wageni mnasahau wazawa.
 
Tungekuwa na hao SIYAVUMA wengi nchini mwetu, hakika nchi yetu ingekuwa na professional players wengi sana. Hongera nyingi ziwafikie kwa kuwawezesha wachezaji wa Kitanzania kwenda kucheza nje ya nchi.
 
Tungekuwa na hao SIYAVUMA wengi nchini mwetu, hakika nchi yetu ingekuwa na professional players wengi sana. Hongera nyingi ziwafikie kwa kuwawezesha wachezaji wa Kitanzania kwenda kucheza nje ya nchi.
Tukiwa na vijana wetu wengi nje ya nchi tunaweza kufanya vizuri kwenye timu ya taifa, hatutakuwa tena kichwa cha mwenda wazimu.
 
Hawa mawakala ndo wanawapoteza hawa watoto.
Ada ya usajili kiasi gani?
Mshahara na manufaa mengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyovyote vile itakavyokuwa ila ligi ya Afrika Kusini ni bora kuliko yetu, exposure ipo ya kutosha muhimu ni dogo atengeneze na kupandisha thamani yake, mengine yatafuata mbele ya safari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…