GE2025 Ally Mshamu: Kwa aliyotufanyia Samia hatakiwi kuomba Kura, Matokeo yake yanaonekana vizuri

GE2025 Ally Mshamu: Kwa aliyotufanyia Samia hatakiwi kuomba Kura, Matokeo yake yanaonekana vizuri

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Ally Mshamu Nampwita, mkulima wa zao la korosho kutoka Kijiji cha Mnavira, Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, amesema mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, hakuwa na sababu ya kuomba kura kwa wananchi wa mkoa huo, kwa kuwa tayari amewatendea mambo makubwa yanayoonekana wazi.

Akizungumza baada ya kusikiliza hotuba ya Dkt. Samia aliyoitoa leo Septemba 23, 2025, Nampwita amesema wananchi wa Mtwara wanaona matokeo ya uongozi wake, ikiwemo upatikanaji wa pembejeo kwa wakati na kwa wingi, pamoja na juhudi za Serikali kutafuta masoko ya uhakika kwa zao la korosho.

Aidha, amesema wakulima wa Mtwara wanaendelea kunufaika na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita, hususan katika sekta ya kilimo na miundombinu, hivyo wana kila sababu ya kuendeleza imani yao kwa Dkt. Samia.
 
Back
Top Bottom