britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 16,295
- 33,994
Picha hii ilipigwa mwaka 1943, wakiwa vitani, India (Vita ya pili ya dunia), hawa ni Moja ya watu muhimu sana katika uanzishwaji wa chama cha TANU. Kushoto ni Ally Sykes (17) ambaye ndiye alikuwa na Kadi No. 2 ya TANU na kulia ni kaka yake Abdulwahid Sykes (19), aliyekuwa na Kadi No. 3. Ikumbukwekwe kadi No. 1 ya TANU ni ya Julius Nyerere.
Kwa sababu ya uwezo wa kifedha ni Ally Sykes ndiye aliyenunua kadi 16 za mwanzo kabisa, kisha akazigawa, alimpatia Mwl. Julius Nyerere kadi No. 1, yeye akajipa No. 2 na kaka yake akampa kadi No. 3.
Alifanya hivo baada ya kujua kwamba Nyerere ana kipawa sana na ni mtu muhimu ambaye anaonekana kuwa mzalendo na aliyajua hayo baada ya Nyerere kumshirikisha kwamba ni bora kuwa na chama kilichoimara zaid kuliko kutegemea chama cha wafanyakazi
Britannica

Mkuu Britanicca, asante kwa picha, ila dataz na dates hazijakaa vizuri kwa sababu
TANU ni Mwalimu Nyerere, na Mwalimu Nyerere ni TANU!.
- TANU ilianzishwa mwaka 7/7/1964 na ndio ile sherehe ya 77, sasa hizi habari za hawa Ndugu wawili watoto wa mpiganaji vita wa Kizulu, alioletwa nchini baada ya kuisha kwa WW 1, yanatokea wapi?!.
- Mwalimu Nyerere ndiye sio tuu ndiye alikuwa Mwenyekiti wa TANU, bali ndiye mwanzilishi wa TANU, sasa kitu uanzishe mwenyewe, halafu unatuletea story za kupewa kadi na Fulani simply because huyo fulani ndio amechapisha hizo kadi, haijakaa vizuri!.
- Ni kweli kina Sykes walikuwa na uwezo kifedha, but they were not the only ones, the richest kwenye Tanu aliuwa ni Mzee John Rupia.
- Naomba nikupe Angalizo, na wewe usijekuwa ni mmoja wa waliolishwa matango pori kuhusu uasisi wa TANU, maana iliwahi kusemwa humu kuwa hata huo uenyekiti wa TANU, Mwalimu alipewa na wale Wazee wa Kariakoo!.
- Iko historia nzuri sana ya TANU iliyoandikwa na Mmmalawi, William Kanyama Chiume (Kwacha) ambayo iliishia kwenye manuscripts, sijui ziliishia wapi, hazikuchapishwa mpaka leo, kilichobakia humu jf, ni watu kututupia picha hizi na zile na kulishana matango pori!.
P