Wadau za Jumapili? Jana nikiwa na ndugu yangu tulipeleka mzigo pale Shekilango kwenye ofisi za Bus la Ally's. Kulitokea sitofahamu kati ya mbeba mizigo mmoja na abiria ambaye na yeye alipeleka mzigo.
Kilichonisikitisha, ni mzozo wao kusimamiwa na matusi kutoka kwa mbeba mizigo huyo kwenda kwa mteja huyo.
Mbeba mizigo alifikia hatua ya kumwambia mteja aulize yeye ni nani pale? Na anaweza kumfanyia kitu kibaya mteja huyo.
Mbeba mizigo huyo ni mrefu, mwembamba ana mwonekano wa 'hana cha kupoteza.'
Kisa; mteja alifika na Bajaj akitaka kushusha mzigo wake. Staff wa Ally's akamwonesha mahali pa kusimamisha Bajaj ili ashushe mzigo wake. Wakati huohuo mbeba mizigo alikuwa analiita basi litoke. Kwa hiyo Bajaj ikafunga njia. Ndipo mbeba mizigo akamuwakia mteja bila kujua mteja alielekezwa na staff.