Almanusura Nanga mmoja anipige risasi mafunzoni JKT...

Almanusura Nanga mmoja anipige risasi mafunzoni JKT...

Kinyonyoke

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
3,498
Reaction score
13,138
Majina ya vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo ya JKT yametangazwa.
Kutangazwa kwa majina haya kumezirudisha nyuma kumbu kumbu zangu yapata miaka miwili sasa.

Tulikuwa Range(Mazoezi ya ulengaji shabaha).Taratibu zote zilizingatiwa kwa umakini wa hali ya juu sana lakin ilipofika zamu yetu (Combania C Coy) kutokana na muda kwenda sana na uchovu makamanda walipungukiwa na umakini kabisa.

Anyway to cut a long story short jamaa aliekuwa pembeni yangu..mikono yake ilikuwa imelegea sana kama mlenda.Sasa wakati anafyatua risasi, SMG yake iliyumba na kuja uelekeo wangu(haikunilenga moja kwa moja lakini kama tu angeligeuka hatua chache ingekuwa story tofauti!) ila risasi ilitua mita kadhaa tu mbele yangu huku ganda la risasi likinichabanga usoni na kuniachia maumivu kiasi.Nilikata moto!

Vijana waende JKT, hawatajutia.Pia mtu anaweza kula shavu MS kama ilivyotokea kwa mshikaji wangu.Who knows?
maxresdefault.jpg
 
🤣🤣😅 mkuu tuendelee ulivyokata moto ikawaje?
 
Sitaki kukumbuka ya JKT, naomba niishie hapa.
 
Acha uongo ganda la risasi haliwezi kutoka kwa kasi hivyo mpaka kukufanya uzimie. Wewe ni nanga kiwango cha brigedia
 
Si ndo nimemshangaa.
Mimi kule mbele target ilikokuwa si kuna digidigi alijipendekeza?asee sitowasahu wale ma mp baada ya zoezi kupita walienda kuchukua asee wakatangulia nae

Maanake ni kwamba "target" uliikosa...!
 
Back
Top Bottom